MKUU WA WILAYA YA ILALA Mhe. SOPHIA MJEMA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS KWA VITENDO

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akitembelea barabara ya Lumumba jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya eneo ambalo wamelitenga kwa ajili ya Wamachinga kufanya biashara zao siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Amewapongeza baadhi ya Wamachinga waliojitokeza eneo hilo na kuwataka wengine kujiandikisha na kuchangamkia fursa hiyo yenye tija kwao. Mhe Dc aliongozana na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Msongela Palela, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni. na Katibu Tawala wa Wilala ya Ilala Edward Mpogolo
 Baadhi ya  wafanyabiashara  wakijiandishi  majini yao ili wapatiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa  na mazingira rafiki, leo jijini Dar es Salam.
 Baadhi ya  wafanyabiashara  waliojitokeza katika eneo hilo  wakiendelea na  kazi 
 Baadhi ya wananchi wakiwa katika barabara ya Lumumba wakijipatia mahitaji yao ikiwa ni moja ya eneo ambalo wamelitenga kwa ajili ya machinga kufanya biashara zao.
Wafanyabiashara  waliojitokeza wakiweka alama katika eneo hilo 
Kufuatia agizo la Rais John Pombe Magufuli kuwataka viongozi kuwatafutia maeno ya kufanyia biashara Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga na ikiwezekana wapewe fursa ya kuzitumia baadhi ya barabara kwa shughuli hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema ameanza kutekeleza agizo hilo kwa vitendo.   
Akiwa mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam  Mkuu wa Wilaya huyo amewapongeza  baadhi ya machinga waliojitokeza eneo hilo lililotengwa kwa ajili yao na kuwataka wengine kujiandikisha na kuchangamkia fursa hiyo yenye tija kwao.

Comments