Tuesday, November 15, 2016

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango azindua tawi la benki ya UBL Kariakoo


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji akikata utepe kuzindua tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika jana. Kulia ni Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain na kushoto ni Afisa Mtenadaji Mkuu wa UBL Tanzania, Faisal Jamall. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya United Bank Limited (UBL) la Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika jana.
Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi la Kariakoo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wa pili kutoka kulia akikata keki maalum katika hafla ya uzindua tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika jana. Kulia kwake ni Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain na kushoto ni Afisa Mtenadaji Mkuu wa UBL Tanzania, Faisal Jamall
Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain(kulia) akimkabidhi tuzo maalum Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji katika hafla ya uzindua tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye tawi hilo jana.
Wageni mbalimbali na wafanyakazi wa benji ya UBL wakifuatilia uzinduzi wa tawi la benki hiyo jana.


Serikali imesema kuwa Tanzania ina fursa nzuri katika uwekezaji wa huduma za kifedha na kuwavutia wawekezaji wa mataifa tofauti na malalamiko ambayo yamekuwa yakienezwa na baadhi ya taasisi hizo hapa nchini. 

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijazi wakati wa ufunguzi wa tawi la jipya la Kariakoo la benki ya United Bank Limited (UBL) Tanzana Limited. 

Hivi kaibuni kulikuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya taasisi za kifedha na kutoa viashiria vya kufirisika, jambo ambali alisema, uzinduzi wa tawi la Kariakoo la benki ya UBL ni ishara tosha kuwa sekta ya uwekezaji wahuduma za kifedha hipo imara na kuendelea kuwavutia wawekezaji. 

Waziri Kijazi alisema kuwa uchumi wa Tanzania kwa sasa unakuwa na bodi ya wakurugenzi wa benki ya UBL imevutiwa nayo na kuamua kuwekeza nchini. Alisema kuwa benki hiyo kwa sasa imetumia jumla ya dola za Kimarekani milioni 32 (Sh 67.2 bilioni) kutoa mikopo kwa wateja wake na huduma nyingine 

“Benki ya UBL Tanzania ilianza rasmi Mwezi Septemba mwaka 2013 na kufanikiwa kupata faida iliyopelekea kuzindua tawi lingine huku ikiwa na mipango ya kufungua matawi kadhaa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Arusha, hii ni ishara tosha kuwa sekta ya huduma ya kifedha Tanzania inakuwa na kupata maendeleo makubwa,” alisema Dk Kijazi. 

Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa UBL Bw. Wajahat Husain alisema kuwa wamefuraishwa na hali ya uwekezaji hapa nchini na kuamua kuwekeza, ikiwa ni tawi la kwanza la benki hiyo kwa bara la Afrika. 

Husain alisema kuwa wameichagua Tanzania kutokana kukuwa kwa uchumi, hali bora ya kisiasa, maliasili na huduma za bandari ya Dar es Salaam ambayo ni kiungo cha wafanyabiashara, si kwa Tanzania tu, bali hata kwa nchi sita jirani. Alisema kuwa kupanuka kwa mtandao wa benki hiyo kwa Dar es Salaam kutaifanya benki hiyo kuwa kiungo muhimu cha masuala ya kiuchumi. 

“Tumefurahi kuwekeza hapa nchini, benki yetu ni miongoni mwa beki kubwa sana nchini Pakistani, tukiwa na matawi zaidi ya 1,300 na kutoa huduma wengi, tumevutiwa na hali ya uwekezaji hapa nchini na muda mfupi tuliowekeza, tumeona matunda yake na kuamua kupanua wigo,” alisema Husain ambaye pia ni Mwenyekiti wa Benki hiyo nchini. 

Alisema kuwa wapo tayari kwa soko la ushindani la hapa nchini na nyenzo yao kubwa ni kutoa huduma za kisasa zenye ufanisi mkubwa.

No comments: