Wednesday, November 09, 2016

WAZIRI NAPE: WADAU WAMICHEZO ACHENI KUKIMBILIA MAHAKAMANI KUTAFUTA SULUHU YA MIGOGORO

Anitha Jonas – WHUSM- Dar es Salaam. 

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa wadau wamichezo nchini kuacha kukimbilia Mahakamani wanapokuwa na migogoro bali watumie vyombo vya kusimamia michezo kutafuta suluh
u. 

Wito ameutoa Leo jijini Dar es Salaam alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu kupata taarifa ya mgogoro wa Chama cha Riadha Taifa (RT) kinachotaraji kufanya uchaguzi hivi karibuni huku baadhi ya wanachama kusikika kususia uchaguzi huo na kusema watakwenda mahakamani,ambapo alikiri kutokuwa na taarifa ya mgogoro huo. 

“Napenda kuwasihi wanamichezo wote kuacha tabia ya kukimbilia mahakamani kwa ajili ya kutafuta suluhu panapokuwepo na migogoro kwani hakuna haja yakufanya hivyo sababu Wizara na vyombo vyake havishindwi kutatua matatizo yao hivyo ni vyema watumie vyombo vyenye dhamana ya kushuhulikia masuala kero zao kama Baraza la Michezo la Taifa (BMT)”,alisema Mhe.Nnauye. 

Akiendelea kuzungumza Mhe. Nnauye alisema kuwa amegunduwa kuwa migogoro mingi katika vyama vya michezo ni hutokana na baadhi ya watu kugombea ulaji na kusababisha kuharibu zoezi la uchaguzi katika vyama vya michezo. 

Pamoja na hayo Waziri huyo aliendelea kuzungumza kwa kutoa ahadi ya kutafuta dawa ya kushughulikia migogoro katika vyama vya michezo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha bunge kinachoendelea Mjini Dodoma. 

Halikadhalika Mhe.Nnauye ameviagiza vyombo vinavyosimamia michezo nchini kufanya kazi ya kutatua migogoro hiyo kwa haraka ili kuboresha michezo na kuondoa sababu za wanamichezo hao kukimbilia mahakamani kwani suala la usuluhishi halipendezi kufanyika mahakamani wakati kuna vyombo vya serikali vya kusimamia michezo pamoja na Wizara.
Post a Comment