Thursday, November 10, 2016

WAZIRI KAIRUKI AKABIDHIWA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA KAMPENI YA KITAIFA YA KUJENGA NA KUKUZA MAADILI

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Bw. Valentino Mlowola taarifa ya utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahama Nyanduga.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akitoa utambulisho kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Bw. Valentino Mlowola akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (katikati) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahama Nyanduga. akitoa neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Bw. Valentino Mlowola (kulia) akijibu swali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki na kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji ya maadhimisho ya siku ya maadili kitaifa mara baada ya Mheshiwa Waziri kuzindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG),Profesa Mussa Assad ,amesema kuwa kwa kipindi cha miaka kumi hadi kumi na tano iliyopita hapa nchini watanzania wengi wamekuwa waongo, hali iliyochangia kuongeza kwa ukosefu wa maadili.

Profesa Assad ameyasema hayo alipokuwa anafunga mkutano wa wandishi wa habari juu ya masuala ya maadhimisho ya siku ya maadili na utawala bora yatakayofanyika Desemba 10 mwaka huu.

“Ndani ya miaka 10 hadi 15 sasa,Watanzania wengi wamekuwa waongo sana kiasi cha kupoteza maadili na uaminifu kwani swala hili la uongo limeshamiiri sana katika matumizi ya simu kiasi cha kuathiri utendaji wetu wa kawaida katika kazi za kila siku”amesema Profesa Assad.

Amesema kuwa hata vyombo vingi vya habari hivi sasa vimeingia katika mpango huo wa kuongopa kwa kushindwa kuandika habri za kina na zilizofanyiwa utafiti ambao unatoa ushahidi wa moja kwa moja kwa jambo linalo andikwa.

 Amemaliza kwa kusema kuwa ni  vyema watu wakaanza kupunguza uongo kwenye simu na Maisha yao ya kila siku hili kuishi Maisha halisi yatakayowezesha kupunguza uovu

No comments: