Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (mbele) akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya maandalizi ya mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania. Kamati hiyo inajumuishwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (CAG). Lengo la kikao hicho ni kujadili maandalizi ya ujenzi wa bomba hilo.
Mratibu Miradi ya Ubia wa Sekta Binafsi na Umma (PPP), Salum Mnuna kutoka Wizara ya Nishati na Madini (kulia) akielezea maandalizi ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanzania katika kikao hicho. Kushoto ni Mjiolojia Mkuu kutoka Wizara hiyo, Adam Zuberi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa akisikiliza majadiliano yaliyokuwa yanaendelea.
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Comments