Tuesday, October 11, 2016

MAENDELEO YA VIWANDA YATATOKANA NA BENKI YA TADB KWA KUWAFIKIA WANANCHI WALIOWENGI-DK.ASHANTU KIJAJI.

 Naibu Waziri wa Fedha, Uchumi na Mpango, Ashantu Kijaji akizungumza wakati uzinduzi wa Bodi ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa TADB, Rosebudy Kurwijila akizungumza katika uzinduzi juu ya majukumu ya bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Ashantu Kijjaji akipokea mfano wa hundi ya Sh.milioni tano kwa ajili ya tetemeko la Ardhi mkoani Kagera leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha, Uchumi na Mpango, Dk.Ashantu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi wa TADB leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MAENDELEO ya Viwanda yanahitaji mali ghafi za kilimo hivyo Benki ya Maendeleo ya  Kilimo nchini (TADB) inawajibu ya kuwafikia wakulima ili matokeo ya viwanda yaweze kuonekana ikiwemo na kuwa na masharti ya riba nafuu au kuondolewa kabisa.

Hayo ameyasema leo Naibu Waziri wa Fedha , Uchumi na Mipango, Dk. Ashantu Kijjaji wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), amesema kuwa sekta ya kilimo inaajiri watanzania asilimia 70 huku ikichangia pato la Taifa kwa asilimia 28 ambayo ni kidogo kutokana na ukuaji wa sekta ambayo inatakiwa kwenda na viwanda ambapo TADB ndio yenye kuweza kuleta mapinduzi hayo viwanda kwa kuwafikia watanzania waliowengi.

Amesema bodi ya wakurugenzi ya TADB inajukumu la kutekeleza na kuboresha sekta ya kilimo kwa kuwafikia watanzania wengi katika maeneo ya kijijini kutokana ni kuwa wazalishaji wa mazao mbalilmbali ambayo ndio yanaweza kuzalisha viwanda na nchi ikaweza kukua kiuchumi pamoja na kuongeza pato la taifa.

Dk. Ashantu amesema benki ya kilimo ihakikishe wanatafuta vyanzo vya fedha ili waweze kukuza mtaji na kutoa mikopo kwa wakulima kwa masharti nafuu katika kumfanya mkulima kuweza kunufaika kilimo chake.

"TADB ina deni kubwa kwa wakulima sasa ni wakati umefika wa bodi kufanya kazi kwa uadilifu katika kuinua sekta ya kilimo kwa kutoa mikopo na sio kwa bodi kufanya mikutano nje ya nchi na kuacha kutatua changamoto ya mikopo katika sekta hiyo" amesema Dk. Ashantu.

Nae Mweenyekiti wa Bodi hiyo, Rosebudy Kurwijla ameiomba serikali kuiwezesha benki ili kuweza kufikia wananchi waliowengi na wanahitaji ya kukopeshwa na TADB katika kuendeleza kilimo.
Amesema kilio cha TADB ni mtaji na bila kufanya hivyo itakuwa ni vigumu kuwafikia wananchi waliowengi.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas Samkyi amesema mpango wao ni kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika  katika kuweza kupata mtaji wa kuweza kuwakopesha wakulima ili kuweza kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.
Post a Comment