MKOA WA SONGWE WAPIGWA JEKI MIFUKO 125 YA CEMENT KUTOKA TPB

Mkuu wa Mkoa wa Songwe (katikati) Luteni Mstaafu Chiku Galawa akipokea msaada wa Cement mifuko 125 yenye thamani ya shilingi mil 2 kutoka kwa benki ya Posta Tanzania (TPB) tawi la Mbeya.kulia aliyevalia T.shart Meneja Benki ya Posta Mbeya Humphrey Julias ,kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo na Meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduma Teddy Msanzi aliyshikana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Songwe. 
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo akishukuru mara baada ya kupata msaada wa Cement1 kutoka benki ya Posta Tanzania (TPB) 
Mkuu wa Mkoa Songwe Picha ya Pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Songwe na wadau mbalimbali . 
BENKI ya Posta Tanzania(TPB) kupitia tawi lake Mkoani Mbeya, imetoa msaada wa mifuko ya saruji 125 thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa serikali ya Mkoa mpya wa Songwe.


Akikabidhi mifuko hiyo , kwa uongozi wa serikali ya Mkoa wa Songwe, Meneja wa benki ya Posta mkoa wa Mbeya, Humphrey Julius amesema benki hiyo iliguswa na suala la ujenzi wa majengo mapya ya ofisi za Mkoa wa Songwe hivyo kuona umuhimu wa kuchangia ikiwa kama faida wanayoipata kutoka kwa wateja wanaowahudumia.

Amesema, mbali na kutoa msaada huo wa mifuko ya saruji, pia benki hiyo imeshakabidhi madwati 130 kwa baadhi ya shule za msingi za Wilaya ya Tunduma, Ileje zilizopo Mkoani Songwe na dawati 30 kwa shule ya Mbeya Day Mkoani Mbeya.Amesema, serikali pekee haiwezi kufanya mambo yote ni lazima wadau zikiwemo Taasisi, Mashirika, Asasi na mtu mmoja mmoja kuingiza mikono yao ili kuipungizia serikali mzigo.

Hata hivyo, akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu Chiku Galawa, aliishukuru benki ya Posta kwa msaada huo, muhimu kwani serikali ya Mkoinahitaji zaidi ya mifuko 50 elfu ya saruji na mabati laki moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo ya ofisi pamoja na shule na Zahanati.

Comments