WADAU WA KITAIFA NA KIMATAIFA WAKUTANA KUJADILI MIFUMO MBALIMBALI YA KISHERIA INAYOSIMAMIA MASUALA YA USAJILI WA MATUKIO MUHIMU YA BINADAMU NA UKUSANYAJI WA TAKWIMU NCHINI.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya katiba na Sheria Bw Amon Mpanyu akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Wadau kutoka Nchini Ghana, Marekani na mashirika ya Kimataifa ya maendeleo waliokutana hii leo Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani kwa lengo la kujadili Mifumo mbalimbali ya kisheria inayosimamia masuala ya usajili wa matukio muhimu ya Binadamu na Ukusanyaji wa takwimu,kulia kwake ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson na kushoto kwake ni Msajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu kutoka Marekani state ya Hawaii Bw Alvin Onaka,pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi Erica Yegela.
Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia kwa umakini majadiliano kuhusu maboresho ya mifumo ya sheria zinazosimamia masuala ya usajili wa matukio muhimu ya maisha ya binadamu katika Hoteli ya Stella Maris Mjini Bagamoya Mkoani Pwani.
Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi ambaye ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amon Mpanju katika Hoteli ya Stella Maris Mjini Bagamoya Mkoani Pwani.

Comments