Saturday, October 08, 2016

WAZIRI NAPE: NGOMA ZA ASILI NI CHANZO CHA AJIRA KWA VIJANA


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( wa pili kulia) akifurahia jambo na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson (kulia) wakati wa KUFUNGA Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016  liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016. 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za kiutamaduni Wwakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016 kulia ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu Mtendaji BASATA Geodfrey Mngereza. 
Kikundi cha Utamaduni cha Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewashauri vijana kutumia ngoma za asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.

Ametoa ushauri huo leo Mjini Mbeya alipokuwa akifunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 na kuwahimiza vijana kutosubiri kuajiriwa ikiwa wanaona wana uwezo wa kufanya kitu ambacho kitawasaidia kupata kipato na kuendesha maisha yao.

“Ngoma za asili ni chanzo cha ajira kwa vijana na sisi kama Serikali tutashirikiana na wadau wa Sanaa na Utamaduni ili kutengeneza ajira na kudumisha mila na desturi za nchi yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.

Aidha kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa fursa pekee kwa vijana kujiajiri kupitia shughuli za Sanaa na Utamaduni kwani ndio sekta ambazo zimetoa ajira kwa vijana wengi duniani kwa sasa.

“Nawashauri vijana wa kitanzania kuangalia na upande huu wa Sanaa na Utamaduni kuna ajira pia na sisi tupo pamoja nao na tutawapa ushirikiano ili wafikie malengo” alisema Mhe. Tulia.

Tamasha hili liliondaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson linafanyika kwa siku mbili na limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili vipatavyo 62 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

No comments: