Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ili kuzungumzia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Katika Mkutano huo Makonda amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza au kuondoa kabisa changamoto zinazowakabili ikiwemo, vibaka, dadapoa na uchafu wa mazingira, akisema, ikiwa wananchi watashitiki kikamilifu ni rahisi kukomesha tatizo la vibaka kwa sababu vibaka na dadapoa wanatoka miongoni mwa familia zao na hali kadhalika uchafu wa mazingira unatokana na takataka wanazozalisha wananchi wenyewe.
Kamanda wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uliofayika leo jioni Buguruni kwa Mnyamani
Viongozi waandamizi katika Wilaya ya Ilala, wakimsikiliza mkuu wa mkoa Paul Makonda wakati akihutubia wananchi katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani leo jioni. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela, Ofisa Tawala wa Manispaa hiyo, Edward Mpogolo, Naibu Meya Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Segerea wilayani humo Bona Kalua
Mjumbe wa Shina namba tano, Katika Kata ya Myamani, Buguruni Zubeda Lugiga, akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara leo jioni
Mkazi wa Buguruni, Sadik Mgaya akieleza changamoto na kero zinazowakabili wananchi wa eneo hilo wakati wa mkutano huo wa Makonda
Comments