Monday, October 10, 2016

EFM YAENDELEA KUSAKA VIPAJI VYA SINGELI

Msaani chipukizi, Jfari Salumu a.k.a Winnero akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.
Msaani chipukizi,Ramadhani Iddi a.k.a Sindano Simba akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa mziki wa nyimbo za singeli wakiendelea kupagawa katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.

Kituo cha EFM kimeendelea na harakati zake za kuwasaidia na kuwainua vijana wanaojihusisha na muziki. Kwa kutumia shindano maalumu la singeli michano linalofanyika kila siku ya jumamosi kuanzia saa nne hadi saa sita mchana, EFM radio inasaka wasanii chipukizi wenye vipaji vya kuimba nyimbo za singeli na baadae kuwaendeleza katika muziki huo. 

Zoezi hili ni endelevu na litadumu kwa muda wa wiki 12 katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam na Pwani ambapo muziki mnene utafika. 

Jumla ya wasanii 5 huibuka na ushindi na washindi hawa hupatikana kila eneo ambapo zoezi hili la kusaka vipaji vipya vya singeli (Singeli Michano) hufanyika. 

Meneja matukio na mawasiliano ya efm redio Neema Mukuarsi amesema baada ya zoezi hili wasani hawa chipukizi watapata nafasi ya kupata semina kutoka kwa TCRA, BASATA na TRA pale Dar live siku ya ijumaa ya tarehe 14.10.2016 saa 8;00 mchana ili waweze kupata elimu ya kulipa kodi,waweze kuimba nyimbo zenye maadili na kuhakikisha nyimbo zao zinakuwa na maadili katika jamii. 

No comments: