Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, Margareth Mpunga, aliyefika kuhudumiwa wakati wa Wiki ya PSPF kwenye kitengo cha huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam, Oktoba 4, 2016. Wakurugenzi na Mameneja wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, waliungana na wafanyakazi wa kitengo hicho kuwahudumia wateja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za wiki hiyo inayofikia kilele Oktoba 7
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa wateja cha PSPF, Laila Maghimbi, (kushoto), akimuhudumia mteja ofisini kwake Oktoba 4, 2016
Judith Mtweve wa kitengo cha mawasiliano (call centre), akiwa kazini
Meneja wa Kitengo cha Hudma kwa Wateja, akimsikiliza mteja
Mkurugenzi Mkuu, akimsikiliza kwa makini mteja
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wamepongeza uongozi wa Mfuko huo, kwa huduma bora na za haraka katika kuhudumia wateja.Hayo wameyasema Oktoba 4, 2016 wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwenye makao makuu ya Mfuko huo jengo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
“Nimefurahishwa na huduma zilizokuwa zikitolewa, kwani nilipofika nimepokelewa na kuhudumiwa haraka, sikuchelewa, kilichonileta ni kuwasilisha risiti za benki za michango yangu,” alisema Mwanachama wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari,(PSS), Hamid Maxan Haidary.
Hata hivyo mwanachama huyo alishauri, Mfuko ufanye juhudi kuelimisha umma hususan wajasiariamali kama yeye wajiunge nao kwani anahakika wengi watajiunga.
“Wafanyakazi wapelekwa huko kwenye kata, najua zipo juhudi kubwa za kufanya matangazo kwenye radio/tv, magazeti na mitandao ya kijamii, lakini sio vibaya wafike wenyewe mitaani kutoa elimu zaidi.” Alishauri.
“Mimi kama mtu mwenye kipato cha chini, nilikuwa Napata shida sana inapokuja swala la kuugua au kuuguliwa na watoto au mke wangu, lakini hivi sasa hilo sio tatizo tena kwangu, kwani kupitia bima ya afya ambayo nimepata baada ya kujiunga na PSPF, ninatibiwa bila wasiwasi.” Alifafanua Haidary.
Mwanachama mwingine wa Mfuko huo ambaye ni mstaafu, Peter Protus Mbele (64), alielezea kufurahishwa kwake na faida anayopata kutoka PSPF yeye kama mstaafu, ambapo licha ya kuchukua pensehni ya kila mwezi, ameweza pia kukopa fedha benki na hivyo kuboresha shughuli zake.
“Kwa ujumla nafurahia huduma za PSPF, nimeweza kupata mkopo benki, panatokea mara chache kuchelewa kwa palipo ya mwezi ya pensheni, lakini mimi nachukulia kama ni changamoto ya kawaida, kwani hata nyumbani mama anaweza kuchelewa kutayarisha chakula, pengine kwa sababu kuni ni mbichi au mkaa hauko vizuri lakini hatimaye chakula kinawiza na mnakula,” alisema.
Naye Devotha R. Kayumbe, aliusifu uongozi wa PSPF kwa kuwajali wateja. “Nimejisikia raha kuhudumiwa na Mkurugenzi Mkuu, hii inaonyesha jinsi watumishi wa umma wanavyowajibika na kwenda sambamba na kasi dhana ya Hapa Kazi Tu.”. Alisema Kayumbe.
Naye Naomi Albert Duma, ambaye alifika kwa nia ya kujiunga na Mfuko kupitia Uchangiaji wa Hiari, (PSS), alisema, ameridhishwa na huduma aliyopata kwani amehudumiwa kwa haraka na hakutegemea kama angechukua muda mfupi kumaliza kile kilichomleta.
“Nimefika kujiunga na PSS, tayari nimehudumiwa na sasa naondoka.”Alisema .
Akizungumzia Wiki ya Huduma kwa wateja, Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha PSPF, Laila Maghimbi, alisema, kila mwaka wiki ya mwanzo ya Oktoba Dunia huadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja. “Kuanzia Oktoba 3 hadi 7 tutakuwa tukiadhimisha wiki hii, kwa viongozi mbalimbali wa Mfuko, kupita maeneo mbalimbali ya nchi kuungana na wafanyakazi wa huko na kuhudumia wateja.” Alifafanua.
Meneja huyo alisema, katika wiki hii wateja pia watapata fursa ya kutoa maoni yao ili Mfuko uweze kuyafanyia kazi kwa nia ya kuboresha huduma, alisema.
Baadhi ya wakurugenzi na mameneja wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, waliungana na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja, ili kutoa huduma kwa wanachama waliofika kupatiwa huduma.Mkurugenzi mkuu alipata fursa ya kutoa huduma kwa muda wa dakika 35 na baadaye kutoa barua za pongezi kwa wafanyakazi bora watatu wa kitengo hicho.
Wafanyakazi hao ni pamoja na Afisa Huduma kwa wateja, January Buretta, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji, Hilda Mwema na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Matilda Nyallu.
Alitolea mfano hapo makao makuu ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Adam Mayingu, naye aliungana na wafanyakazi wa kitengo chake kuhudumia wateja.
“Sambamba na kutoa huduma, lakini pia Wiki hii tutaitumia kuwatunukia wafanyakazi wetu bora katika kitengo hiki.” Aliongeza
Mkurugenzi Mkuu, akimsikiliza Mteja, Devotha Kayumbe,Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Laila Maghimbi, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mkurugenzi Mkuu, akimkabidhi barua ya pongezi, Mmoja kati ya wafanyakazi watatu bora wa ,kitengo hicho, January Buretta, ambaye ni Afisa mwandamizi Huduma kwa wateja wa PSPF
Mkurugenzi Mkuu akimkabidhi barua ya pongezi, Afisa Mkuu wa Matekelezo, Matilda Nyallu
Mkurugenzi Mkuu akimkabidhi barua ya pongezi, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji, Hadija Mwema
Mkurugenzi wa Uendeshaji, wa PSPF, Neema Muro, (kulia), akifuatilia jinsi Afisa Uendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, Zeinab Dau, (wapili kulia), wakati akimuhudumia mteja
Meneja Matekelezo wa PSPF, Francis Mselemu, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani, Sosthenes Mushema, (kulia), akimsikiliza kwa makini mteja aliyefika kuhudumiwa Oktoba 4, 2016
Afisa mwandamizi msaidizi wa nyaraka, Gwamaka Ngomale, (kushoto), akimuhudumia mteja
Wateja wakipatiwa huduma na wafanyakazi wa PSPF
Wafanyakazi wa PSPF, sehemu ya call centre wakitekeleza wajibu wao
Picha ya pamoja
Paulina Kagaruki, (kulia), Afisa uendeshaji, akimhudumia mteja
Isack Kimaro, (kushoto), akimuhudumia mteja
Afisa wa Uendeshaji wa PSPF, Elizabeth Shayo, akimuhudumia mteja Oktoba 4, 2016
Hadji Jamadary (kulia), akimuhudumia mkuu wa wilaya wa zamani Lephy Gembe, aliyefika kupata huduma za PSPF Oktoba 4, 2016
Afisa Mkuu Huduma kwa Wateja wa PSPF, Queen Edward, (kulia), akimuhudumia mteja
Comments