Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, Ernest Makale, akitoa taarifa ya kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na jeshi hilo kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Na BMG
Makale ameeleza kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kujipatia kiasi cha shilingi 240,000 kati ya shilingi 500,000 alizokuwa ameomba kutoka kwa mmoja wa walioomba kujiunga na JWTZ.
Amebainisha kwamba mtuhumiwa mmoja ambaye ni mstaafu wa JWTZ aitwaye Sophia Chacha amekuwa akimsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na jeshi ambapo ili kupata nafasi hiyo mtuhumiwa amekuwa akihitaji kiasi cha shilingi 500,000.
Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 10 mwaka huu katika hoteli moja iliyopo Kirumba Jijini Mwanza kufuatia mtego wa maofisa wa TAKUKURU.
"Kitendo cha mtuhumiwa kujifanya afisa wa jeshi hakihusiani na makosa yaliyo chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namaba 11/2007, hivyo jalada lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa wakili wa serikali mfawidhi ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili". Alifafanua Makale.
Aidha Makale ameongeza kwamba TAKUKURU wilayani Misungwi imemfikisha mahakamani Katibu wa Idara ya Utumishi wa Waalimu TSD wilayani humo kwa kosa la tuhuma za kupokea rushwa shilingi 400,000 kutoka kwa Kitoki Mgaya ili asimchukulie hatua za kinidhamu kazini.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, Ernest Makale, akitoa taarifa ya kwa wanahabari kuhusu kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Mtuhumiwa Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ.
Kushoto ni mtuhumiwa Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ. Kulia ni Sophia Chacha ambaye ni mstaafu wa JWTZ anayetuhumiwa kumsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na JWTZ.
Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza
Comments