BODI YA MFUKO WA BARABARA YASITISHA UFADHILI WA UJENZI WA BARABARA KWA MANISPAA YA KINONDONI

 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB), Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.
uje2
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Mfuko huo Bw. Eliud Nyauhenga.
uje3
Baadhi ya Watendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB) wakimsiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Bw. Joseph Haule (hayupo pichani), wakati alipotoa ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni.Jijini Dar es Salaam


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Bodi ya Mfuko wa Barabara umesitisha ufadhili miradi ya barabara kwa Manispaa ya Kinondoni baada kubainika kutengeneza barabara chini ya kiwango pamoja na ukiukaji sheria za manunuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Joseph Haule amesema kusitisha ufadhili kwa barabara kwa Manispaa ya Kinondoni kumetokana manispaa hiyo kujenga barabara chini ya kiwango ikiwemo Barabara ya Masjid-Quba iliyopo Sinza.

Haule amesema barabara barabara hiyo mkandarasi anafanya kazi huku Bodi ikiwa imetoa Sh.Bilioni 3.3 lakini Manispaa imemlipa Mkandarasi sh.milioni 200 ambapo ni kinyume na sheria ya manunuzi ya kulipwa sh.milioni 801 kwa mkupuo wa kwanza.

Amesema barabara hiyo ilitakiwa kuisha mwaka jana, lakini bado wanaendelea kujenga ambapo ni kinyume cha mkataba na kuhoji kuwa mkandarasi huyo anaendelea kujenga kwa mkataba gani wakati muda wake wa ujenzi ulikuwa umeisha.

Bodi imeuagiza Katibu Mkuu wa Tamisemi kuwachukulia hatua wote waliohusika na mkataba wa barabara ya Masjid Kuba pamoja kubadili mfumo manispaa jinsi kuweza kufanya fedha ya serikali inayotengwa na Barabara inakuwa salama.

Aidha bodi hiyo imetaka Halmashauri zote kuhakikisha zinasimamia fedha za barabara ipasavyo na pamoja na barababaea kujengwa kwa ubora unaotakiwa..

Comments