TIMU ZA SIMBA NA YANGA MARUFUKU UWANJA WA TAIFA-SERIKALI


 Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akiwa amekaa akiangalia jinsi viti vilivyong’olewa katika Uwanaja wa Taifa na Serikali   kuchukua uamuzi wa kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa na kuzuia mapato ya mechi waliyocheza mpaka watakapolipa fidia  kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na Serikali kufikia  uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimini iliyofanyika mara baada ya mechi wa jana kati ya Simba na Yanga na jumla ya mageti manne yamevunjwa na viti1781 vimeong’olewa katika Uwanja wa Taifa.
  Eneo liliong’olewa viti katika Uwanja wa Taifa katika mechi ya Simba na Yanga iliyofanyika Oktoba Mosi.Habari na Picha na Raymond Mushumbusi - MAELEZO
Timu za soka za Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa miumbombimu ya Uwanja  wa Taifa yakiwemo mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.

Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akikagua na kutembelea maeneo yalioathirika na uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba na Yanga katika mechi iliyochezwa Octoba Mosi 2016 katika Uwanja wa Taifa.
Mhe. Nape Nnauye ameongeza kuwa wameendaa mfumo wa kutumia kamera Uwanjani ili kubaini makosa yatakayokuwa yanafanyika ili kuzuia vitendo vya kihualifu na uharibifu katika Viwanja vya michezo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa wamesikitishwa sana na uharibifu ulitokea katika mechi ya Simba na Yanga na kusababisha uharibifu wa viti na mageti ya kuingilia Uwanjani.

Ameongeza kuwa kwa tathimini iliyofanyika mageti manne yameng’olewa na mashabiki kwa upande wa Simba na Yanga na pia kwa upande wa ndani jumla ya viti 1781 vimeng’olewa katika upande wa mashabiki wa Simba.
“Mara nyingi tumekubaliana kutunza Uwanja huu kwa ajili ya matumizi ya watanzania wote na kama wasimamizi tunasikitika kwa kitendo hiki kilichotokea na tujue kuwa ni kodi za wananchi ndio zilitumika kujenga Uwanja huu na pia ndizo zitazotumika kukarabati Uwanja tuwe na tabia ya kupenda na kutunza vya kwetu.

Klabu za Simba na Yanga zimekuwa na ushindani mkubwa katika soka la Tanzania na kumekuwa kukitokea mambo mbalimbali pale timu hizo zinapokutana ikiwemo uharibifu wa miundombinu katika Viwanja na vurugu kwa mashabiki pale mmoja wao anapofungwa.

Comments