Tuesday, November 03, 2009

Binti wa miaka 11 ajifungua mtoto siku ya harusi


SOPHIA, BULGARIA
Msichana mdogo mwenye umri wa miaka 11 kutoka nchini Bulgaria wiki iliyopita alijikuta akiwa mama baada ya kujifungua mtoto wake siku ya sherehe ya ndoa yake na kijana mdogo mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni baba wa mtoto huyo.
Kordeza Zhelyazkova alikuwa bado amevalia gauni lake la harusi pamoja na taji yake wakati akiwasili hospitalini na kujifungua mtoto wa kike aliyempa jina la Violeta.
Msichana huyo alijihisi kuwa ana mimba wiki mbili baada ya sikukuu yake ya kuzaliwa. Alijifungua wiki iliyopita akiwa na mumewe pembeni aliyejitambulisha kwa jina la Jeliazko Dimitron.
Kordeza alijifungua salama mtoto wa kike mwenye uzito wa kilo 2.4 ambaye alimpa jina la Violeta lakini alitoroka hospitali na mtoto wake usiku huo huo aliojifungua mtoto wake ili awahi kumalizia sherehe za harusi yake.
Binti huyo alisema hataki tena kuendelea na shule na anataka atumie muda mwingi kucheza na mtoto wake.
Kordeza ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi, alisema kuwa alikutana na mumewe mpya kwenye viwanja vya michezo vya shule yake baada ya Jeliazko kumuokoa kutoka kwenye kipigo cha wahuni wa mitaani.
Kordeza anadai alianza kufanya mapenzi na Jeliazko bila kutumia kondomu na anakiri alikuwa hajui kondomu ni kitu gani wakati huo.
Kordeza alipata mimba ndani ya wiki moja baada ya kuanza kufanya mapenzi na mpenzi wake huyo.

1 comment:

John Mwaipopo said...

Hebu pata nukuu hii:

"lakini alitoroka hospitali na mtoto wake usiku huo huo aliojifungua mtoto wake ili awahi kumalizia sherehe za harusi yake".

Nukuu hiyo hapo juu inaonyesha moja ya madhara ya mimba za utotoni. Ona sasa anawaza sherehe zaidi kuliko afya yake na mtoto wake huyo.

Swali la pili ni kwa jinsi gani wahusika wa sherehe hiyo waliruhusu na kuandaa ifanyike. Au torari za nchi yao zinaruhusu. Makubwa.

tatu 'sauti ya baragumu' inampongeza kwa kujifungua salama. kwa umri wake hili lilikuwa jambo la harari ya kukaribia kupoteza maisha.