Monday, November 09, 2009

Tamko kuhusu Hali ya Kisiasa huko Zanzibar

Tumepokea vyema taarifa kuwa viongozi wa vyama vikuu viwili vya siasa visiwani Zanzibar wamekutana na kujadili kuhusu “haja ya kudumisha amani, maelewano na ushirikiano miongoni mwa Wazanzibari wote.”

Kwa muda mrefu tumekuwa tukitoa wito kwa viongozi wa kisiasa wa Zanzibar kutetea na kusimamia siasa za maendeleo, amani na haki ili pasiwe na Mzanzibari yeyote anayejihisi kuwekwa pembezoni katika kuwa na sauti kuhusu ueandeshaji wa serikali yake na pasiwe na Mzanzibari yeyote anayekuwa na hofu ya kudhuriwa kutokana na msimamo wake wa kisiasa.

Ni matarajio yetu kuwa kama sehemu ya kuendeleza nia njema ya mkutano huu, viongozi wa Zanzibar watachukua hatua mahsusi za kujenga mazingira mazuri ya kisiasa visiwani Zanzibar yatakayowezesha kukua kwa utawala bora na maendeleo ya kiuchumi kwa wote. Hatua ya kwanza itakuwa ni kwa viongozi kuwaelekeza wanachama wao kujizuia dhidi ya vitendo vyote vya utumiaji nguvu na uvunjifu wa amani.

Tunaunga mkono maono ya viongozi hawa wawili kwamba iwapo Zanzibar inaweza kutanzua tatizo la mgawanyiko wa kisiasa lililodumu kwa miongo kadhaa, basi ubunifu, ujasiri na moyo wa kujituma wa watu wa Zanzibar utajidhihirisha wazi kwa manufaa ya Wazanzibari wote, ndugu zao wa Tanzania na hata katika ukanda wote wa Afrika Mashariki na kwingineko.

Zanzibar imetoa mchango mkubwa katika utamaduni wa dunia. Ni wakati mwafaka sasa, kwa mara nyingine tena, Wazanzibari wakaidhihirishia dunia kile wanachoweza kufanya na kukifikia.

No comments: