Tuesday, November 03, 2009

Muhimbili sasa imebadilika




HOSPITALI ya Taifa Muhimbili inafanyiwa mabadiliko makubwa hebu cheki hapa reception pamoja na jengo la Chuo kikuu cha Muhimbili, kwa kweli ipo hatua kubwa suala ni kwamba je tutaweza kumaintain standard ya juu kiasi hiki.Jana Rais Jakaya Kikwete amewataka watanzania kutoenda kutibiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili wakitokea majumbani mwao bali waende baada ya kupata rufaa za hospitali za wilaya na rufaa.
Rais alitoa kauli hiyo jana wakati waziara yake iliyoambatana na ufunguzi wa kitengo cha matibabu ya Figo.
“Muhimbili inapaswa kuwa ni hospitali ya kutibu magonjwa makubwa yanayoweza kupelekwa nje ya nchi,lakini magonjwa ya kawaida yanapaswa kutibiwa katika hospitali ya Wilaya pamoja na Zahanati”alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Hii ni hospitali ya rufaa inayopokea wagonjwa kutoka hospitali zingine si kila mgonjwa anapaswa kutibiwa hapa wengine watibiwe kwenye hospitali zilizoko jirani na maeneo wanakoishi wagonjwa”.
Rais pia lisema kuwa lengo la serikali ni kuwapatia wananchi huduma bora ya afya na ndiyo maana hivi sasa kuna sera ya kuijenga vituo vya afya na zahanati jirani na makazi ya wananchi.
Kuhusu hatua ya watanzania kwenda kutafuta matibabu ya nje ya nchi Rais Kikwete alisema serikali inaendelea kufanya jitihada za kuboresha huduma ya afya nchi ili wananchi wasiende kutibiwa nje ya nchi.
“Hakuna haja ya watanzania kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa sababu hivi sasa tunajitahidi kuboresha huduma ya afya nchini kadri ya uwezo wetu katika hospitali hii ya muhimbili”:
“Nimeelezwa kuwa hivi sasa kunakitengo cha matibabu ya Figo hapa Muhimbili hivyo watu wanaohitaji kubadilisha damu watapa huduma hiyo hapa hakuna haja ya kwenda Kenya au India kwa ajili ya kubadilisha damu”alifafanua Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa “Hapo nje tumeonyeshwa ramani ya majengo mawili makubwa yanayojengwa na wachina yatakapo kamilika yatatumika kwa ajili ya upasuaji wa moyo”.
Mbali na ufunguzi wa kitengo hicho cha Figo Rais pia alifungua jengo jipya ya kitengo cha matibabu ya dharura liyofunguliwa na taasisi ya misaada ya kibinadam ya ‘Abbott Fund’.Imeandikwa na Jackson Odoyo.

1 comment:

Anonymous said...

imebadilika jengo, huduma vipi?