Rais Kikwete Mbeya


Mmmiliki wa kiwanda cha kukata mawe mjini Mbeya cha Marmo Granito Mines Limited Bwana Firoz Jessa akimwonesha Rais Jakaya Mrisho Kikwete aina mbazlimbalzi za mawe ya Marumaru yanayozalishwa na kiwanda hicho wakati Rais kikwete alipotembelea kiwanda hicho kukagua ujenzi unaoendelea na mitambo mbalimbali.Pemebeni nia mke wa rais Mama Salma Kikwete.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL Bwana Robin Goetzsche akimwonesha Rais Jakaya Mrisho Kikwete mitambo ya kisasa ya kuzalisha bia muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho mjini Mbeya leo mchana.Kushoto ni meneja wa kiwanda hicho Bwana Calvin Martin.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe lamsingi katika kiwanda cha Tanzania Breweries Limited (TBL) Tawi la Mbeya leo mchana.Kushoto anayepiga makofi ni Mwenyekiti wa Bodi ya TBL Waziri Mkuu mstaafu David Cleopa Msuya na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Bwana Robin Goetzsche.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dr.Harun Machibya akimuongoza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kukagua baadhi ya majengo ya hospitali hiyo jana muda mfupi baada ya Rai Kuweka jiwe la msingi katika hospitali hiyo leo mchana(picha na Freddy Maro0

PC-Rais Kikwete akishuka kwenye ngazi mara baada ya kuzindua huduma ya gari linalotembea kutoa huduma katika kituo cha afya cha elembo Mbeya vijijini alipodhuru kata hiyo na kuzungumza na wananchi.

Comments