Wednesday, October 31, 2012
Tuesday, October 30, 2012
Usafiri wa Treni Dar es Salaam waanza Rasmi
USAFIRI wa
kutumia treni jijini Dar es Salaam kutokea eneo la Ubungo Maziwa
kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni ya Treni) umeanza jana . Treni ya kwanza imeondoka Ubungo majira ya saa 12:00 asubuhi
kuelekea katikati ya jiji, ambapo kwa mujibu wa maofisa wa Shirika la
Reli Tanzania (TRC) imetumia wastani wa dakika 30 kufika katikati ya
jiji.
Treni
ilioanza kazi jana iliyokuwa na injini mbili (vichwa vya traini) moja
ikiwa imefungwa nyuma na nyingine mbele huku ikiwa na mabehewa sita,
yaani matano ya abiria wa kawaida (watu wazima) na moja likiwa ni
maalumu kwa ajili ya kubeba wanafunzi. Abiria mmoja ni sh. 400 kwa tripu
huku wanafunzi wakitakiwa kulipa sh. 100 kwa kila mmoja.
Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndiye aliyezindua usafiri wa leo ambao
ni wamajaribio, akiwa pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka
ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi
Kitengo cha Reli.
Treni hiyo
pia imezinduliwa pamoja na treni ya TAZARA ambayo itafanya kazi kama ya
Ubungo, lakini yenyewe ikianzia eneo la TAZARA kuelekea Mwakanga.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi huo Waziri Mwakyembe alisema
atahakikisha treni hiyo inaendelea kufanya kazi ili kuwasaidia kiusafiri
wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisumbuliwa na kero ya
usafiri hasa kwa foleni, ambapo utumia muda mrefu njiani kuingia na
kutoka jijini.
Alisema
jumla ya mabehewa ya treni 14 pamoja na injini mbili zimekarabatiwa na
mafundi wazalendo nchini, ambayo ndiyo yatakayokuwa yakifanya kazi ya
kusafirisha abiria kuingia na kutoka jijini kila asubuhi na jioni.
Alisema kwa sasa inafanya treni moja kwa majaribio lakini baada ya
uzinduzi mkubwa zitafanya kazi treni mbili, na zitakuwa zikipishana
njiani moja ikirudi na nyingine ikienda.
Akifafanua
zaidi alisema kitendo cha mafundi wazalendo kufanya ukarabati kwa
mabehewa na injini kimeokoa kiasi kikubwa cha fedha za umma kwani
ukarabati wote umetumia sh. bilioni 2.1 tu, ilhali kama Serikali
ingelazimika kukodi injini gharama ingekuwa kubwa zaidi kwani bei ya
kukodi injini moja ya treni ni sh. milioni moja kwa siku.
Hata
hivyoDk. Mwakyembe amewataka Watanzania hasa abiria kuwa wavumilivu kwa
upungufu utakaojitokeza kwa safari za mwanzo kwani bado wanaendelea
kufanya marekebisho kadhaa, lakini baada ya muda mambo yatakaa sawa.
Mwandishi
wa habari hizi alikuwa ni mmoja wa wasafiri walioizindua treni hiyo leo.
Awali akizungumza mmoja wa viongozi waandamizi wa TRC, alisema treni
hiyo itafanya kazi kila siku isipokuwa kwa siku za jumapili na siku kuu
na itaanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa sita mchana na kupumzika hadi saa
9:00 za jioni, itakapoendelea tena na safari zake hadi majira ya saa
nne usiku.
Uchunguzi
uliofanywa na muandishi wa habari hizi umebaini kuwa behewa moja la
treni linauwezo wa kuchukua abiria 66 wakiwa wamekaa, lina milango
minne, feni, taa, muziki/redio, pamoja na mikanda maalumu ya kujishikia
kwa abiria ambao watakuwa wamesimama.
Aidha mabehewa yote yana madirisha ya kutosha kuingiza na kutoa hewa ya
kutosha.
Treni
ilioanza kazi leo, ikitokea Ubungo ilikuwa ikisimama vituo vya eneo la
Mwananchi (relini), Tabata Relini, Buguruni Miamani, Tazara, Kariakoo
Gerezani (Kamata), na mwisho Kituo Kikuu cha Treni kilichopo jirani na
Kituo cha Polisi Kati (Katikati ya Jiji).
Abiria wa Usafiri wa Treni uliozinduliwa rasmi jana kwa ajili ya safari za ndani ya Jiji la Dar wakipanda usafiri huo.
Abiria Wakisubiri Treni Kituoni.
Treni ikiwa safarini.
Abiria wakiwa ndani ya Treni hiyo huku wakiwa ni wenye furaha na usafiri huo.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha
Reli wakati wa uzinduzi wa Safari za Treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam jana.
Waziri wa
Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akiwa nadni ya treni hiyo sambamba na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na viongozi waandamizi kutoka
TRC, Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha
Reli wakati wa uzinduzi wa Safari za Treni ndani ya Jiji la Dar es
Salaam jana. SOURCE:MICHUZI
SIKU YA IBADA YA KUOMBEA AMANI KWA TAIFA MCH. DK RWAKATARE AIBUKA NA UJUMBE MZITO
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima
wa Moto Mikocheni Mh. Dkt. Getrude Rwakatare akitoa Ujumbe kwa
Watanzania waliohudhiria Ibada Maalum ya Kuliombea Taifa ambapo ametaka
watu kutobaguana kwa misingi ya Dini, Ukabila wala Siasa na kusema
pamoja na Utawala bora pia tunahitaji maombezi ili tuweze kufikia
Malengo yaliyokusudiwa kulipeleka Taifa linapotakiwa kufikia.
Dkt. Rwakatare amesema nia kubwa ya
kufanya Ibada hiyo ya Maombezi ni kutaka kuweka usawa kutokana na siku
za hivi karibuni kuibuka kwa Matamko mbalimbali kutoka kwa watu tofauti
wakiwemo viongozi wa Kitaifa, Kidini na wa baadhi ya Makundi
yanayohitilafiana na kusema tukiomba kwa jina la Mungu kila kitu
kitakwenda kama tulivyomuomba ili Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani
na Utulivu kama ilivyokuwa miaka yote ambayo ni kimbilio la watu wa
Mataifa mbalimbali kwa sababu Watanzania hawajui kuchukiana na wamekuwa
watu wa kushikamana kwa miaka yote.
Picha Juu na Chini ni Waumini
waliohudhiria Ibada Maalum ya kuliombea Taifa wakinyanyua bendera juu
kuimba na kuabudu kwa furaha bila kuonyesha tofauti ya matabaka.
Msanii wa Kimataifa wa muziki wa
nyimbo za Injili wa Tanzania Rose Muhando akiimba na kumtukuza Mungu
sambamba na wachezaji wake wakati wa Ibada hiyo maalum ya kuliombea
Taifa letu liendelee kuwa na Amani, Upendo na Utulivu.
Nimeonja Utamu wa Yesu Weeeeee........!!!
Mchungaji Kiongozi Dkt. Rwakatare akijumuika sambam
Monday, October 29, 2012
Chadema yailiza CCM udiwani
Mpaka sasa matokeo ya kata 14 yalnaonyesha kuwa CCM imerejesha kata zake saba, huku CHADEMA ikinyakua kata sita, ambapo mbili zilikuwa za kwao na nne imewanyang’anya CCM na CUF ikiwa na kata moja.
Matokeo
Wakati hali ikiwa hivyo, matokeo ya udiwani katika baadhi ya kata yalikuwa yakiendelea kutolewa huku CHADEMA ikiendelea kuiliza CCM kwa kuzitwaa baadhi ya zilizokuwa kata zake.
Jijini Arusha katika Kata ya Daraja Mbili, CCM ilipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyozoa kura 2192 dhidi ya 1315 za chama tawala.
CHADEMA wameweza kuzirejesha kata zao mbili za Nangerea jimboni Rombo, ambapo mgombea wao Frank Sarakana alijizolea kura 2370 dhidi ya 1134 za Dysmas Silayo wa CCM pamoja na ile ya Mtibwa, mkoani Morogoro.
Wilayani Sikonge katika kata ya Ipole, CCM walipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyopata kura 577 dhidi ya 372 za washindani wao, na vilevile kuitwaa kata nyingine ya Lengali wilayani Ludewa iliyokuwa ya CCM.
CHADEMA pia ilikuwa ikiongoza katika kata ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, hadi tunakwenda mitamboni usiku.
Nayo CCM ilifurukuta kwa kuzirejesha kata zake za Msalato ya mkoani Dodoma, Bang’ata ya Arumeru Magharibi kwa kuwa 1177 dhidi ya 881 za CHADEMA, Mletele ya Songea CCM ilishinda kwa kura 950 na CHADEMA ilipata 295.
Pia CCM iliweza kutetea kata zake za Mwawaza mjini Shinyanga, Lwenzela mkoani Geita, Bungala wialayni Kahama na Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuibwaga CHADEMA wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilishinda kata ya Newala.
Sunday, October 28, 2012
CCM YAIBWAGA CHADEMA BUGARAMA, KAHAMA
Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa
kuibwaga Chadema katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika katika
Kata ya Bugarama wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Habari zilizopatikana zimesema, katika uchaguzi huo ulifanyika leo CCM imepata kura 1145
Chadema: 772 na TADEA: 156 wagombea wakiwa Nixon Igoko (CCM) Erasmus Francis (Chadema) na Clement Michael (TADEA)
Pia habari zilizopatikana kutoka Kata ya
Shinyanga mjini ambako pia uchaguzi mdogo wa Udiwani umefanyika,
zinasema CCM imeshinda. Hata hivyo hatukuweza kupata mizania ya ushindi
huo kwa kura.
SOURCE: http://bashir-nkoromo.blogspot.com/2012/10/ccm-yaibwaga-chadema-bugarama-kahama.html
Friday, October 26, 2012
RAIS DK SHEIN ASHIRIKI SALA YA EID EL HAJJ
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine
wakijumuika na waislamu na wananchi katika swala ya EID el Hajj
katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine
wakijumuika na waislamu na wananchi katika swala ya EID el Hajj
katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Baadhi ya Waislamu na wananchi wakisikiliza Hotuba,baada
ya Swala ya Eid el Hajj iliyotolewa na Sheikh Soraga,katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
ya Swala ya Eid el Hajj iliyotolewa na Sheikh Soraga,katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na waumini ya Dini ya
Kiislamu baada ya kuswali swala ya EID el Hajj katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na waumini ya Dini ya
Kiislamu baada ya kuswali swala ya EID el Hajj katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mzee wa Mshitu wishes you all the best on Eid al Adha
The Management and Staff of Mzee wa Mshitu Blog would like to congratulate all Muslims all over the World for successful celebrations of Eid Al Adha.
We would like to assure our esteemed readers and viewers of Mzee wa Mshitu Blog will strive to serve you better by bringing you current and well- researched news, analyses and photos by our competent staff.
MAKAMU WA RAIS DKT. GHARIB BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MSIKITI MPYA WA JIHAD WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal,
akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Msikiti mpya wa Jihad, baada ya
kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya
Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa Sikukuu ya
Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko
wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na
Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal,
akijumuika na waumini wa Dini ya Kiislam
katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya
wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa
Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo
na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji
fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya
Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja wa waumini wa Kiislam wa Kijiji cha Vuchama wakati akiondoka eneo hilo baada ya kuzindua na kuweka Jiwe la Msingi na kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. leo Oktoba 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi na waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka eneo hilo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Wednesday, October 24, 2012
UMOJA WA MATAIFA WATIMIZA MIAKA 67
Waziri wa
Afrika Mashariki akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja wa Mataifa
ikiwa ni ishara ya kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo katika viwanja
vya Karimjee jijini Dar leo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Meja Jenerali Raphael Muhuga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Tanzania
katika sherehe za maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu
kuzaliwa kwake.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta akiwasili katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam leo katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja
wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 67 tangu uanzishwe.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaa leo.
Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati) akimtambulisha
Mh. Samwel Sitta kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali ya
Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Waziri wa Afrika Mashariki
Mh. Samuel Sitta akipokea heshima ya wimbo wa Taifa baada ya kuwasili
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo kuhudhuria kilele
cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa baada ya kutimiza miaka 67
ya UN tangu kuanzishwa.
Mh. Samuel Sitta akikagua gwaride maalum katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Dkt. Alberic Kacou, Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meha
Jenerali Raphael Muhuga wakiwa Meza kuu.
Pichani Juu na Chini ni viongozi wa
Madhehebu ya Dini nchini wakiomba Dua kwa ajili ya kubariki sherehe za
kutimiza miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 67
tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam, Sitta aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa kuisaidia
Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza
umaskini.Waziri Sitta alisisitiza kwamba bado Umoja wa Mataifa
unakabiliwa na changamoto nchini kama vile amani na usalama, tatizo la
njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa silaha za maangamizi.
Katibu wa UNA Tanzania Fancy Nkuhi akizungumza kwenye hafla hiyo alisema umoja wa mataifa
imefanya kazi kubwa katika kuwaunganisha vijana wa bara la Afrika.
Nkuhi alisema kupitia YUNA walitoa elimu ya afya ya uzazi na ugonjwa wa
Ukimwi kwa vijana katika mikoa kumi hapa nchini Tanzania katika harakati
ya kuelimisha vijana madhara ya ugonjwa huo na afya ya uzazi kwa
vijana.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa
kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium Schools) ambao walikuwa
kivutio wakati wa maadhimisho ya miaka 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania wakiwa katika gwaride maalum kupamba sherehe hiyo.
Meza kuu ikifurahia jambo wakati wa
gwaride la watoto wa shule ya Heritage baada ya kuonyesha mbwembwe
katika kupamba sherehe hiyo.
Mauzo ya Nyumba za Mindu
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UUZWAJI WA NYUMBA ZA MRADI WA UJENZI WA MINDU, DAR ES
SALAAM
Kwa mara nyingine tena Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) leo 24 Oktoba, 2012 limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi
wake mpya wa Mindu, jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huu ulianza rasmi mwezi
Novemba mwaka 2011, na unatarajiwa
kukamilika rasmi Aprili 2013 na mteja kuweza kukabidhiwa nyumba yake mwezi
Mei 2013, ikiwa ni miezi 18 baada ya
kuanza ujenzi.
Mradi unatarajiwa kugharimu kiasi cha
zaidi ya Shilingi bilioni 11 mpaka utakapomalizika, fedha zinazogharamiwa na
Shirika kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo fedha za mikopo ya benki.
Mradi huu uliopo mtaa wa Mindu eneo la Upanga, takribani mita
100 kutoka Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili, una sehemu ya nyumba 60 za kuuzwa
zilizopo kwenye majengo pacha ya ghorofa 15, uko sehemu zenye huduma zote
muhimu za kijamii zikiwamo hospitali,
shule, maduka, na masoko.
Pia Mradi unatarajiwa kuboresha maisha ya
wanunuzi wa nyumba hizi kwani upo karibu kabisa na katikati ya jiji na kwamba
mnunuzi anaweza kwenda kazini bila kutumia gharama yoyote ya usafiri wa
gari. Aidha, nyumba zipo ndani ya uzio
kwa ajili ya usalama wa wakaazi wake na
kuna maegesho ya magari ya kutosha.
Nyumba 60 tu zinazouzwa ambapo kila nyumba ina vyumba vitatu
vya kulala, vyo vinajitegemea. Kila nyumba ina ukubwa wa mita za mraba 141 (sq.m),
sebule iliyoungana na eneo la kula chakula, choo cha umma, jiko kubwa la kisasa
na eneo la kufulia na kuanikia nguo.
Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo
maalum la kukusanyia taka, sehemu iliyotengwa maalum kwa ajili ya kufanyia
mazoezi (gym), bwawa la kuogelea (swimming pool) na eneo kubwa la ziada la
maegesho ya magari.
Kila nyumba itauzwa kwa bei ya TZS
272,050,673.08 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT ) na TZS
321,019,794.24 ikiwa na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
Tunawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wote walio
nchini na nje ya nchi kujitokeza ili kununua nyumba hizo. Wanaweza kufanya
mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika, Ofisi zetu za Mikoa au kupitia barua
pepe na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato
ulio wazi wa manunuzi.
Katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa
nyumba, Shirika linajenga nyumba za gharama ya juu, kati na chini ili
kuwahudumia watanzania wa kada zote. Katika azma hiyo, nyumba 10,000
zitakazojengwa kufikia 2015 zitahusu watu wa
kipato cha juu na nyumba 5,000 zitakazojengwa kufikia mwaka huo zitakuwa
ni nyumba za watu wa kipato cha chini.
Shirika limeanza kujenga nyumba za gharama ya
kati na juu ili kupata faida itakayoliwezesha kuwajengea watu wa kipato cha
chini nyumba za gharama nafuu. Hii inatokana na ukweli kuwa Shirika halipati
ruzuku toka serikalini ya kujenga nyumba kwa ajili ya wananchi wa kipato cha
chini. Mradi huu wa Mindu tunaouzindua hii leo, ni moja ya miradi ya ujenzi wa
nyumba za watu wenye kipato cha juu..
Ukiwa mdau na mnunuzi
mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua nyumba katika mradi huu, tafadhali
waweza kutumia akaunti nambari : …….. au wasiliana na Kitengo cha Mauzo simu namba 0754 444 333; barua pepe:
sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya Shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAZINDUA MAUZO YA NYUMBA ZA MAKAZI MINDU PLACE
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Mindu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu, kulia kwake ni Meneja wa Masoko na Utafiti wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Itandula Gambalagi.
Meneja wa Masoko na Utafiti wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Itandula Gambalagi (kushoto) akibadilisha mawazo na bwana Stanley wa Aggrey and Clifford ambao ni wadau wakubwa wa matangazo na utafiti wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za
makazi za Mindu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David
Misonge Shambwe (kulia) akizungumza na vyombo vya habari kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza
za makazi za Mindu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu.
Baadhi ya watu waliofika kushuhudia uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Midu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu.
Nyumba hizo za makazi zinavyoonekana kwa ndani
Wadau muhimu wa sekta ya habari wakifuatilia kwa kina maelezo ya Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe (hatyupo pichani) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Mindu zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu. (Picha zote kwa hisani ya SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA)
RAIS JK AKUTANA NA MWALIMU WAKE
PICHANI NI MATUKIO MBALIMBALI YA RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOKUTANA NA MMOJA WA WALIMU WALIOMFUNDISHA UDSM MIAKA YA 1970, PROF. ABDUL AZIZ JALLOH. WAWILI HAO WALIKUTANA BAADA YA MIAKA MINGI WAKATI RAIS AKIZINDUA ZOEZI LA TATHMINI YA UTAWALA BORA CHINI YA MPANGO WA AFRIKA KUJIPIMA KIUTAWALA BORA (APRM) MACHI, 2012 IKULU DAR ES SALAAM. PROF. JALLOH ALIKUWA NCHINI AKIWA MMOJA WA WATAALAMU BINGWA WALIOKUJA KUHAKIKI HALI YA UTAWALA BORA NCHINI. MWENYE 'FRENCH TIE' NI WAKILI (BARRISTER) AKERE MUNA ALIYEKUWA KIONGOZI WA JOPO LA WAHAKIKI HAO.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Dkt Kikwete Akoshwa na Ushiriki wa Wadau Binafsi Kwenye Miradi ya Maendeleo, Aipongeza Benki ya NBC
Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akikabidhi tuzo maalum kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pil...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...