Kombe la dunia lawasili nchini






Kombe la Dunia la fifa na Coca-Cola limewasili jioni hii na kupelekwa moja kwa moja kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kombe hilo liliwasili nchini majira ya saa 10:30 jioni na kupokelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendela kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa.

Kombe hilo lilopo kwenye safari ya kuelekea Afrika Kusini ilikuwa hapa nchini kwa siku mbili, leo walitakuwa visiwani Zanzibar na kesho Jumamosi ilitakuwa uwanja wa Taifa na kushudia na mashabiki mbalimbali wa mchezo wa soka hapa nchini.

Watu waliojitokeza kwenye uwanja wa ndege walibaki wakiduwa wasijue nini kinaendelea baada ya ndege kuwasili, na kushitukia tayari limeshangia kwenye magari maalumu yalioandaliwa na msafara kuanza ukiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Helkopta.

Akizungumza muda mfupi baada ya kupokea kombe hili Rais Jakaya Kikwete alisema kuwasili kwa taji hilo ni jambo la kihistoria, imeleta changamoto kubwa kwenye maendeleo ya michezo hapa nchini.

"Kutwaa Kombe la Dunia ni ndoto ya kila mchezaji na kufika kwa taji hili Tanzania ni bahati ya pekee kwa kutimiza malengo yetu ya soka," alisema.

Rais alisifu uteuzi wa vijana kwenye timu taifa ya Tanzania kwani unasaidia kuibua vipaji vipya ambao wataweza kusaidia nchi siku za usoni.

Comments

Anonymous said…
Bonjour, charaz.blogspot.com!
[url=http://esviagra.fora.pl/ ]comprar viagra [/url] [url=http://viagraespana.fora.pl/ ]comprar viagra en espana[/url] [url=http://viagraes.fora.pl/ ] viagra en espana[/url] [url=http://viagramedica.fora.pl/ ]vendo viagra en espana[/url] [url=http://viagrasinreceta.fora.pl/ ] viagra online[/url] [url=http://farmaciaviagra.fora.pl/ ]vendo viagra [/url]

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri