Tuesday, April 21, 2009

Deci sasa mapande mapande


WANACHAMA wa tassisi Development Entrepreneurship Community Intiatives (Deci) wameonekana kupoteza mwelekeo baada ya kugawanyika katika makundi mawili, moja likiwa likitaka kuishtaki taasisi hiyo na jingine likitaka kufungua kesi dhidi ya serikali.

Vikundi hivyo, vikiwa na mitazamo tofauti, vinasema vinakamilisha taratibu za kisheria ili kufungua kesi mahakamani.

Mwenyekiti wa kamati ya wanachama wa Deci, Mchungaji Isaack Kalenge, ambaye juzi alikamatwa na polisi na baadaye kuachiwa, aliiambia Mwanachi kuwa taratibu za kuishitaki serikali zimefikia hatua za mwisho na kwamba wakati wowote watakwenda Mahakama Kuu kitengo cha biashara kufungua kesi ya madai.

Alisema serikali haikuwa na sababu za kuifunga Deci kwa sababu hakuna mwanachama hata mmoja aliyekwenda kulalamika serikalini kuwa amedhulumiwa haki zake.

“Hapa kila mtu alikuwa anapata haki yake... imekuwaje serikali kuja kuifunga,” alihoji Mch Kalenge.

Lakini kikundi kingine kimeshafungua jalada la kesi ya madai katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam dhidi ya taasisi hiyokikidai kimepoteza imani na Deci. imeandaliwa na Geofrey Nyang’oro na Patricia Kimelemeta na Picha ya Silvan Kiwale wa Mwananchi.

No comments:

TANZANIA NA URUSI ZAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KATIKA SEKTA YA UCHUKUZI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Shirikisho la Urusi zimeingia hatua mpya ya ushirikiano wa maendeleo baada ya kus...