Masikini Deci



UONGOZI wa taasisi ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (Deci), umetangaza kusitisha huduma ya kupanda na kuvuna katika matawi yote nchini hadi hapo mgogoro uliopo utakapopatiwa ufumbuzi.

Taarifa kutoka mikoa yote ambako Deci ina matawi zinaeleza kuwa katika ofisi za taasisi hiyo yalibandikwa matangazo kuwa huduma hiyo imesitishwa kwa muda ingawa jijini Dar es Salaam walisema imesitishwa kwa siku moja.

Uamuzi huo wa uongozi wa Deci, umetangazwa siku moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuonya kuwa kuwekeza fedha katika taasisi hiyo ni hatari kwa wanaowekeza humo.

Hata hivyo, taarifa hiyo imewakera baadhi ya wateja wa taasisi hiyo waliofika katika ofisi za taasisi hiyo kujua hatima ya fedha zao, huku baadhi yao wakionya kuwa kauli hiyo ya serikali inawaonea wenye kipato cha chini ambao wamedai wamekuwa wakifaidika na Deci.

Mkoani Mwanza taasisi hiyo ilitangaza kusitisha huduma zake hadi itakapokamilisha mazungumzo na serikali.

“Tumefunga utoaji huduma mpaka hapo tutakapokamilisha mazungumzo na serikali,” lilisomeka tangazo lililobandikwa katika ofisi za tawi hilo zilizopo katika jengo la Bima ya Taifa (NIC) barabara ya Posta mjini Mwanza. Kwa taarifa zaidi soma Mwananchi.

Comments