hotuba ya rais Kikwete ya machi 2009

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
KWA WANANCHI, 31 MACHI, 2009

Ndugu wananchi,
Kwa mara nyingine tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata nafasi ya kuzungumza na taifa katika utaratibu wetu wa kila mwezi. Naomba radhi kuzungumza nanyi leo badala ya jana kwa sababu ya shughuli za ugeni wa Gavana-Jenerali wa Nchi rafiki ya Australia, Mama Quentin Bryce aliyetutembelea kuanzia tarehe 30 Machi na kuondoka leo asubuhi.
Leo napenda kuzungumzia mambo matatu. Jambo la kwanza ni mwenendo wa mvua na hali ya chakula nchini. Jambo la pili ni hali ya upatikanaji na uzalishaji umeme nchini. Na, la tatu ni mkutano wa Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani au maarufu kwa jina la G-20 kwa lugha ya Kiingereza. Mkutano unaoanza kesho mjini London, Uingereza.

Mwenendo wa Mvua
Ndugu Wananchi,
Kwa kawaida hii ingekuwa wiki ya pili katika msimu wa mvua za masika kwa maeneo yanayopata mvua hizo. Mvua ambazo hunyesha kwa wingi na kwa saa nyingi mfululizo. Wakati mwingine hunyesha kwa siku mbili au hata tatu mfululizo.
Soma hotuba hii kwa urefu zaidi kwa kubonya hapa chini

Comments