Thursday, April 23, 2009

Zuma mambo safi


JOHANNESBURG, Afrika Kusini

Chama tawala nchini Afrika Kusini, Africa National Congress, ANC tayari kinaelekea kupata ushindi mkubwa, licha ya wasiwasi wa awali kuwa chama kipya cha Congress of the people au COPE kingetingisa ANC.

Jacob Zuma naye yupo kileleni kuwa rais mpya wa Afrika Kusini- hadhi ya juu ya kiongozi ambaye alikuwa amezongwa na mashtaka ya ufisadi wiki mbili tu kabla ya uchaguzi huu.

Matokeo ya awali baada ya kuhesabiwa kwa kura milioni sita yanaonyesha ANC imepata aslia mia 65 ya kura.

Tume ya uchaguzi nchini humo imesema aslia mia 77 ya watu walipiga kura katika uchaguzi wa jana. Katibu mkuu wa ANC Gwede Montasha anaeleza kuwa ANC itajibidiisha kuwatumikia raia wa Afrika Kusini.

Chama cha ANC hata hivyo kimepata upinzani mkubwa katika mkoa wa CAPE Magharibi. Chama rasmi cha upinzani cha Demokratic Alliance kinachoongozwa na Hellen Zille kimepata aslia mia 55 ya kura hadi kufikia sasa.

Matokeo ya awali yanakipa chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu na hivyo kutoa nafasi kwa Jacob Zuma kuwa rais wa nchi hiyo.
Wafuasi wa ANC wamealikwa kusherehekea ingawa kuna kila dalili chama hicho kitashindwa kupata theluthi mbili ya kura zinazohitajika kwa ajili ya marekebisho ya katiba.

Huku robo ya kura zote zikiwa zimekwishahesabiwa, ANC kimejizolea asilimia 65 ya kura na chama cha Democratic Allience(DA) chenye upinzani mkubwa na ANC kimepata asilimia 19 ya kura.

1 comment:

Anonymous said...

weka basi habari za uchaguzi bondeni!
kwanini njia wanaotumia wao na sisi tusiitumie. kwani ni nzuri.

tunatakiwa kujua idadi ya viti vya bunge na idadi ya wapiga kura halafu tunagawanya kujua kila kiti cha bunge ni kura/kula ngapi.

halafu watu wanakwenda kupiga kura..
/kula!

hakuna kampeni za wagombea viti vya ubunge ni uraisi na chama tuuuuuuu
rushwa itaungua na gharama pia.
hapo imekaaje??

nadhani tutaondokana na majimbo yale ya zenj yenye wapiga kura 10,000 wakati kule njombe kuna jimbo la zaidi ya 100,000

..kwa namana hiyo utaona mbunge mmoja wa bara ni sawa na wabunge zaidi ya 5 wa zenji...

wadau mnasemaje???

heri mimi sijasema!
http://www.sowetan.co.za/News/Article.aspx?id=987257