RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA


RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa Nchini. Mabadiliko hayo yamehusisha Wakuu wa Mikoa kumi na moja (11)

Lengo la mabadiliko haya ni kutoa msukumo zaidi wa shughuli za Serikali. Wakuu wa Mikoa waliobadilishwa vituo vya kazi ni hawa wafuatao:-

JINA KITUO CHA SASA KITUO ANACHOHAMISHIWA
1. Mhe. Kanal (Mst) Enos Mfuru Kagera Mara

2. Mhe. Lt. Col. Issa Machibya Mara Morogoro

3. Mhe. Maj.Jen.(Mst) Said Kalembo Morogoro Tanga

4. Mhe. Mohamed Abdulaziz (Mb) Tanga Iringa

5. Mhe. Hajat Amina S. Mrisho Iringa Pwani

6. Mhe. Dkt. Christine Ishengoma Pwani Ruvuma

7. Mhe. Monica Mbega (Mb) Ruvuma Kilimanjaro

8. Mhe. Mohamed Babu Kilimanjaro Kagera

9. Mhe. Abbas Kandoro Dar es Salaam Mwanza

10. Mhe. Eng. James Msekela Mwanza Dodoma

11. Mhe. William Lukuvi (Mb) Dodoma Dar es Salaam


Imetolewa na:


Mhe. Aggrey D. J. Mwanri (Mb).
NAIBU WAZIRI
OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI) – DAR ES SALAAM

15 Aprili, 2009

Comments