Kupima ngoma sasa poa

SERIKALI ya Marekani itatumia zaidi ya Sh10 bilioni za Kitanzania katika kupambana maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na kuboresha huduma za afya katika Jeshi la Polisi, Magereza na Idara ya Uhamiaji.

Hayo yalisemwa jana na mwakilishi wa Shirika la Watu wa Marekani (Usaid), Elise Jensen katika ufunguzi wa kituo cha kupima VVU na kutoa ushauri nasaha (VCT na CTC), kilicho jengwa kwa ushirikiano wa shirika la Pharm Access Foundation na mashirika mengine ya kimataifa.

“Serikali ya marekani imetenga kiasi cha Dola 8.8 za Kimarekani katika kupambana na maambukizi ya VVU pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ukimwi ili kupambana na ugonjwa huo katika Jeshi la Polisi, Magereza na Idara ya Uhamiaji mpaka kufikia mwaka 2010,” alisema Jensen.

Alisema pia kuwa ujenzi wa kituo hicho pamoja na ukarabati wa maabara ya hospitali ya jeshi hilo umegharimu kiasi cha Dola 150 za Kimarekani.


Aliongeza kuwa mpaka kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa vituo hivyo katika kanda na mikoa yote Tanzania, wastani wa watu 200,000 watapata ajira.

Naye mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema alisema tatizo la Ugonjwa huo polisi ni kubwa.

Mwema alisema maabaraba hiyo iliyopo katika Hosipitali Kuu ya Polisi iliyo pembezoni mwa Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam itasaidia katika kupunguza tatizo hilo polisi. Taarifa imeandaliwa na mdau Freddy Azzah wa Mwananchi.

Comments