Monday, July 28, 2025

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUFUNGUA CHAN2024 KWA MKAPA

 






 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024, yanayotarajiwa kuanza rasmi Agosti 02, 2025 katika  Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Amebainisha hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali  Gerson Msingwa Julai 28, 2025 jijini Dar es Salaam  wakati akikagua  maandalizi ya Ufunguzi huo.

Amesema kuwa, nchi 5 za Afrika ambazo ni Burkinafaso, Algeria, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Maurtania, Madagascar tayari zimeanza kuwasili kuanzia  Julai 28,2025.

"Kabla ya uzinduzi huo, uwanja  utapambwa na burudani za  Mziki ambazo zitahusisha wasanii wa Singeli (CHAN SINGELI FEST) ambalo litafanyika nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, bila kiingilio,  kuanzia Julai 30 hadi 31, 2025" alisema Msigwa.  

Ameongeza  kuwa, mashindano hayo ni moja ya maandalizi  ya kuelekea kuwa wenyeji wa AFCON 2027,  hivyo  ni nafasi nzuri ya kufanya maandalizi ikiwemo kuwakaribisha wageni kwani njia za kuingia  nchini zimerahisishwa.

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...