Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda amewataka wataalamu wa sekta ya ardhi kutoa elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya mfumo wa e-Ardhi Kwa kutumia njia mbalimbali kama vile kuandaa mabonanza au matamasha.
"Tuifanye kazi kama ibada Kwa kuhakikisha tunawahi na kufanya kwa weledi na ufanisi wakati Wote".amesema.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ametoa kauli hiyo tarehe 3 Juni 2025 katika kikao cha watumishi wote wa sekta ya ardhi kutathmini hali ya utekelezaji majukumu ya sekta Kwa mwaka 2024/25 na kujipanga namna Bora na yenye ufanisi zaidi ya kutekeleza majukum ya mwaka 2025/26.
Aidha, amewataka wataalam wa sekta ya ardhi katika mkoa huo kuwa wabunifu katika Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi ili kuongeza kasi ya ufanisi wa sekta.
Pia amewataka wataaalam hao kuacha kuzalisha migogoro mipya ya ardhi na kuhakikisha migogoro iliyopo inashughulikiwa.
"Tuendelee utaratibu wa Kliniki za Ardhi kwenye Wilaya na ngazi ya mkoa, tuongeze kasi ya ukusanyaji maduhuli Kwa kuwafuatilia wadaiwa wa Kodi ya Pango la ardhi Kila mara na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria" amesema.
Kwa upande wake Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza Wilson Luge amesema, ofisi yake katika kipindi cha mwaka mmoja wa 2024/2025 imesajili jumla ya Hatimilki za kimila (CCRO) 1,642 sawa na 8.2%.
Kwa mujibu wa Luge, jumla ya Hatimilki 4,665 sawa 10% zimetolewa huku viwanja 9,607 sawa na 33.79 vikiwa vimepimwa na michoro Tp 176 sawa na 176% imeandaliwa.
Akigeukia ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa wake, Bw. Luge alisema, ofisi yake imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 8.5 sawa na 42% .
No comments:
Post a Comment