Saturday, July 26, 2025

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS WA K-FINCO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMAENDELEO

 













Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Fedha na Ujenzi la Korea (Korea Infrastructure Finance Corporation - K-FINCO), Dkt. Eun-Jae Lee, leo tarehe 26 Julai 2025, Ikulu Chamwino, Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili fursa mbalimbali za ushirikiano baina ya Tanzania na Korea ya Kusini, hususan katika nyanja za miundombinu, fedha, na uwekezaji. Ujumbe wa Dkt. Lee umeonesha nia thabiti ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya barabara, bandari, makazi na miundombinu ya kijamii.

Rais Samia amesisitiza dhamira ya Serikali kuendelea kushirikiana na wadau wa kimataifa wanaoonesha utayari wa kuisaidia Tanzania katika kukuza uchumi, kutoa ajira, na kuboresha maisha ya Watanzania.

Mazungumzo haya ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Korea ya Kusini, na yanatarajiwa kufungua milango ya ushirikiano zaidi katika sekta mbalimbali.

#TanzaniaYaViwanda
#UwekezajiTanzania
#SamiaSuluhu
#KFincoTanzania
#Dodoma2025
#MiundombinuNaMaendeleo

No comments:

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKITUNUKIWA NISHANI YA HESHIMA YA JUU YA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI (THE GRAND CORDON)

Dar es Salaam, 14 Agosti 2025  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Nish...