Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 30, 2025, ameweka historia kwa kuzindua rasmi Kiwanda cha Majaribio cha Uchenjuaji wa Madini ya Urani kilichopo Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma.
Akibonyeza kitufe maalum kuashiria uzinduzi huo, Rais Samia amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuhakikisha madini yote nchini, ikiwemo urani, yanachakatwa hapa hapa nchini kwa manufaa ya Watanzania wote. Ameongeza kuwa kiwanda hiki kitasaidia kuongeza thamani ya madini, kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo husika, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kitaifa.
Uwekezaji huu ni sehemu ya mpango mpana wa kukuza sekta ya madini kwa njia endelevu na salama, huku Serikali ikidhamiria kuhakikisha usimamizi bora wa rasilimali za taifa unawanufaisha Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo.
Wananchi wote wanahimizwa kuendelea kufuatilia taarifa rasmi na matukio mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii:
📍 Instagram: @mamakajatz
📍 Twitter/X: @mamakajatz
📍 Facebook: Mama Kaja TZ
📍 YouTube: Mama Kaja TZ
#MamaKaja #KaziIendelee #MadiniNiMaendeleo #TanzaniaYaViwanda
No comments:
Post a Comment