Wednesday, July 23, 2025

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA DAWA NA ZANA ZA KILIMO NCHINI BELARUS





WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, leo tarehe 22 Julai 2025, ameendelea na ziara yake rasmi nchini Belarus kwa kutembelea maeneo muhimu ya uzalishaji na ushirikiano wa kimkakati. 

Akiwa katika mji wa Minsk, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kiwanda cha Belmedpreparaty, ambacho ni maarufu kwa utengenezaji wa dawa za binadamu.

Aidha, Waziri Mkuu pia alitembelea kiwanda cha Minsk Tractor Plant, ambacho kinajihusisha na utengenezaji wa matrekta na mitambo ya kisasa ya zana za kilimo. Ujumbe wa Tanzania ulijionea teknolojia ya hali ya juu inayotumika katika uzalishaji wa vifaa hivyo.

Wakati wa ziara hiyo, pamoja na viongozi wengine, Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Cosato Chumi.

Mheshimiwa Majaliwa pia aliweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Jamhuri ya Beralus.

Kwa ujumla, ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Tanzania kuimarisha mahusiano ya kimataifa kwa manufaa ya wananchi, hasa katika sekta muhimu za maendeleo kama afya na kilimo

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...