Na Mwandishi Wetu Paris, Ufaransa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, akiwa nchini Ufaransa jana Julai 8, 2025 amekutana na Mwandishi wa kitabu cha "Tanzano-Therapie", Prof. Chantal Henry ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Paris East Creteil (UPEC) na mtaalamu wa magonjwa ya afya akili nchini Ufaransa.
Prof. Huyo ameandika Kitabu hicho kinachozungumzia kwa undani jinsi mtu anavyoweza kupona changamoto za saikolojia ya akili na kuhuishwa kisaikolojia kwa kutembelea maeneo ya hifadhi na kuangalia wanyama na vitu vya asili utafiti uliofanywa nchini Tanzania.
“Nilitembelea maeneo mengi ya kiutalii Tanzania hasa Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro mpaka kule Gombe-Mahale nikiwa na familia kisha nikarudi kama mtafiti ambapo nilishiriki mimi mwenye na kuona tiba hiyo lakini pia nimefanya mahijiano na watalii wengi.
“Nikahitimidha kwamba utalii wa kwenda maeneo hayo ya Tanzania unatoa tiba kwa mtu mwenye hatua mbalimbali za magonjwa ya akili na hata saikolojia ya kawaida. Tanzania ni tiba na nimekuwa nikizunguka maeneo mengi huku Ulaya kulisema hilo na watu wameitikia kuja Tanzania,” alisema Prof. Chantal.
Akizungumza mara baada ya mazungumzo na Profesa huyo kuhusu kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kifaransa, Waziri Pindi amesema kitabu hicho kitaendeleza kuitangaza Tanzania na kuunga mkono kazi kubwa anayoifanya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya utalii kupitia filamu ya “Tanzania: The Royal Tour” na “Amazing Tanzania.”
Profesa Chantal akifundisha Chuo Kikuu cha East Central Paris na akiwa pia na kliniki ya kutibu watu wenye changamoto ya afya ya akili, amechapisha maandiko zaidi ya 300 ikiwemo makala mashuhuri ya “Don't Forget the Benefits of Empathy”
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi amesema wana mshawishi Profesa huyo Kitabu hicho kitatafsiriwe pia katika lugha mbalimbali ili watalii kutoka maeneo yote duniani waweze kukisoma na kuelewa ikiwemo Kiingereza na Kiswahili.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Bw. Ali Mwadini ambaye ameeleza kuwa tayari kitabu hicho kwa mara ya kwanza kilizinduliwa Ubalozini hapo Juni mwaka huu.
Waziri Chana na ujumbe wake wapo mjini Paris kuhudhuria Mkutano wa 47 wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya Unesco ambapo taarifa mbalimbali za hali ya uhifadhi wa maeneo ya wanyamapori na malikale zikiwemo za Tanzania, zitawasilishwa
No comments:
Post a Comment