Thursday, July 10, 2025

TANZANIA NA COMORO ZAENDELEZA USHIRIKIANO WA KISWAHILI KWA KUANZISHA MAZUNGUMZO YA KUFUNDISHA LUGHA HIYO MASHULENI












Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, ametamka kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) katika kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Lindi, Mhe. Victoria amesema mashirika hayo ni wadau muhimu wa maendeleo na ni mkono wa pili wa Serikali katika kuwafikia wananchi, hasa katika maeneo ya huduma za jamii kama afya, maji, elimu na mazingira.

“Niseme kuwa NGOs ni mkono wa pili wa Serikali katika kuleta maendeleo kwa jamii, hivyo tutaendelea kuweka mazingira wezeshi ili mshiriki ipasavyo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali,” alisema Mhe. Victoria.

Aidha, amesisitiza kuwa mashirika hayo yanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo, hasa matakwa ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi kwa kila robo mwaka na mwaka mzima, pamoja na mikataba ya kifedha.

“Tufuate sheria na kanuni zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yetu, hasa tunaposhirikiana na mamlaka mbalimbali kwenye sekta kama afya, maji, elimu na mazingira, ili kuhakikisha kuna uratibu mzuri wa utekelezaji wa miradi,” aliongeza Mhe. Victoria.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Bi. Fransisca Mwendesha, alisisitiza kuwa Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na mashirika hayo kwa jamii, lakini ameyataka kuendelea kuzingatia misingi ya kisheria na kiutawala ili kuimarisha mazingira ya utekelezaji wa shughuli zao.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Bw. Jasper Makala, alieleza kuwa Baraza hilo linaendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya sekta ya NGOs na Serikali. Amehimiza mashirika yote kuzingatia sheria na taratibu ili kutimiza malengo ya shirika na mchango wa pamoja katika maendeleo ya Taifa.

Jukwaa hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali, viongozi wa Serikali, na wadau wa maendeleo, ambapo liliongozwa na kaulimbiu isemayo:
“Tathmini ya Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa 2020/2021–2024/2025: Mafanikio, Changamoto, Fursa na Matarajio.”

Jukwaa hilo ni sehemu ya majukwaa ya ngazi ya Halmashauri, Mikoa na Taifa, yanayolenga kufanya tathmini ya mchango wa mashirika hayo katika utekelezaji wa maendeleo ya kitaifa, huku yakitambua fursa na changamoto zilizopo kwa ajili ya kupanga mwelekeo wa baadaye.

No comments:

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AMALIZA ZIARA YA SIKU MOJA MKOANI MBEYA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), leo ameondoka Mkoani Mbeya baada ya kukamilisha zi...