Tuesday, July 15, 2025

VIJIJI VYA LUNG'WA NA NDING'HO WAKABIDHIWA HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA












Zaidi ya Hati 523 za Haki Miliki za Kimila zimegawiwa kwa wananchi wa Vijiji vya Lung'wa na Nding'ho, vilivyopo Kata ya Mwaswale, Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.

Ugawaji huo umefanyika kupitia ushirikiano kati ya Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS), Hifadhi ya Taifa Serengeti, Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Simiyu pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.

Kupitia mpango huo, vijiji husika viliandaliwa mipango ya matumizi bora ya ardhi, hatua ambayo imerahisisha utoaji wa Hati za Kimila kwa wananchi kwa lengo la kuwawezesha kumiliki ardhi yao kisheria, kuimarisha usalama wa miliki na kuhimiza maendeleo endelevu.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi pamoja na Msajili wa Hati Msaidizi Mkoa wa Simiyu wameongoza zoezi hilo la ugawaji wa hati, wakisisitiza umuhimu wa matumizi bora ya ardhi kwa maendeleo ya jamii na uhifadhi wa mazingira.


 

No comments:

πŸ”΄πŸ”΄TABORA ZOO YAENDELEA KUNG'ARA KAMA KITOVU CHA ELIMU, BURUDANI NA UTALII WA NDANI

Na Mwandishi wetu, Tabora. Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) imeendelea kujipambanua kama kivutio muhimu cha elimu na burudani jiji...