Saturday, July 05, 2025

WANANCHI 216 WAKABIDHIWA HATI MILIKI WILAYANI MASWA










Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Simiyu, leo imeendesha zoezi la kugawa jumla ya hati miliki 216 kwa wananchi wa Wilaya ya Maswa. Tukio hilo limekuwa sehemu ya mkakati endelevu wa Serikali katika kuhakikisha kila mwananchi anamiliki ardhi kisheria, kwa usalama na kwa manufaa ya sasa na baadaye.

Zoezi hilo pia linaendelea kuwa chachu ya kuhamasisha umiliki halali wa ardhi, sambamba na kuimarisha usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Wananchi waliopokea hati hizo wameelezea furaha yao na kueleza kuwa sasa wana uhakika wa kuwekeza kwa uhuru na kuondokana na migogoro ya ardhi.

No comments:

WANANCHI 216 WAKABIDHIWA HATI MILIKI WILAYANI MASWA

Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Simiyu, leo imeendesha zoezi la kugawa jumla ya hati miliki 216 kwa wananchi wa Wilaya ya Maswa....