Sunday, July 20, 2025

RAIS SAMIA AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA MISS WORLD LIMITED

Mshindi wa Miss World 2025, Bi. Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand

 Miss World Africa, Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo ya kihistoria na uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited ukiongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu Bi. Julia Evelyn Morley, pamoja na mabinti waliopata heshima ya taji la dunia – akiwemo Mshindi wa Miss World 2025, Bi. Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand na Miss World Africa, Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia. Mazungumzo haya yalifanyika Kizimkazi, Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025.

Katika kikao hicho, ambacho pia kilihudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na viongozi wa sekta ya Maliasili na Utalii, yamejadiliwa maono ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kimataifa ya Miss World 2026. Hatua hii inatarajiwa kuipa Tanzania nafasi ya kipekee ya kuonesha utajiri wa urithi wa kitamaduni, mandhari ya kuvutia na vivutio vya kipekee vya utalii mbele ya macho ya dunia.

Kwa Tanzania, hii ni zaidi ya mashindano ya urembo. Ni fursa ya kimkakati ya kutangaza utalii, kuimarisha taswira ya taifa, kuvutia uwekezaji na kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii na burudani.

“Tunataka dunia ije Tanzania, kushuhudia uzuri wake wa asili, urithi wa utamaduni na ukarimu wa watu wetu,” alisema Rais Samia katika mazungumzo hayo.

Kwa kuwa mwenyeji wa Miss World 2026, Tanzania inajipambanua kuwa kitovu cha Afrika cha matukio makubwa ya kimataifa, ikijenga msingi wa kudumu kwa sekta ya utalii na burudani yenye ushindani wa kimataifa.

#Tanzania2026 #MissWorld2026 #RaisSamia #BeautifulTanzania #Zanzibar #TanzaniaUnforgettable #VisitTanzania #AfricaShines #SamiaEffect #MissWorldAfrica

No comments:

TANZANIA YAWANIA FURSA YA KUWA MWENYEJI WA MISS WORLD 2026 – RAIS SAMIA AONGOZA MAZUNGUMZO YA KIHISTORIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 Bi. Opal S...