Tuesday, July 15, 2025

RAIS MWINYI AWASILI JIJINI ARUSHA






Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili Jijini Arusha leo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika, unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha – AICC.

Mheshimiwa Rais Mwinyi ameondoka Zanzibar mapema leo na kuwasili salama katika Uwanja wa Ndege wa Arusha, ambako amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Kenani Laban Kihongosi, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, na maafisa kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wa mkoa huo.

Mkutano huo wa Afrika unalenga kujadili nafasi ya vyombo huru vya habari katika kukuza demokrasia, uwajibikaji na utawala bora barani Afrika.

No comments:

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AIPONGEZA TANAPA KWA KULINDA MALIASILI NA KUITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango , ameipongeza kwa dhati Shirika la Hifadhi za Taifa Tanza...