Friday, July 07, 2017

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi wakiwa katika Msiba wa Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu, Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akishiriki katika Dua ya kumuombea Marehemu Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo.
 Sehemu ya Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge pindi ulipowasili nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo tayari kwa maandalizi ya mazishi.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza machache.
Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata akisoma taarifa fupi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.

No comments: