Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua chumba cha upasuaji kilichopo katika moja ya kituo cha Afya wilayani Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika hospitali ya wilaya ya Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua majengo ya kutolea huduma katika Hospitali ya Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki katika hospitali ya wilaya ya Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Frank Bahati katika ukaguzi wa miradi ya Afya.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Afya wilayani Ukerewe.
…………………………………………………….
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewajia juu Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya(DMO), Afisa Manunuzi, na mwakilishi wa Mweka hazina wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe baada ya kushindwa kutoa ufafanuzi sahihi juu ya ununuzi wa dawa chini ya mfuko wa Afya wa pamoja (Busket Fund).
Akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo, Jafo amefika kwenye hospitali ya wilaya ya ukerewe na kuwaomba wananchi waliokuwepo hospitalini hapo kueleza changamoto wanazozipata wanapofika hospitalini hapo.
Kufuatia changamoto walizoeleza wananchi, Jafo alionyesha kukerwa kutokana na maafisa hao kushindwa kujibu hoja ya wananchi waliokuwa wakilalamika kwamba wanapofika kwenye hospitali hiyo mara nyingi wataalam wamekuwa na kauli mbaya sambasamba na kukosa dawa.
Jafo aliwageukia wataalam hao kwa kuwauliza ni kiasi gani cha fedha za basket fund wamepokea kwa mwaka Fedha 2016/2017 na kiasi gani kilitumika kununua dawa na vifaa tiba.
Kutokana na Jafo kuhoji fedha hizo, wataalam hao wote walishindwa kufahamu, jambo lililomkera Naibu Waziri Jafo.
Alisema ameshangazwa na kitendo cha wataalam wahusika kushindwa kutambua mambo ya msingi ambayo wanapaswa kuyasimamia ili kutatua kero ya afya kwa wananchi.
Jafo aliwajulisha wananchi kuwa halmashauri yao imepokea jumla ya sh.milioni 727.4 ambapo 33% ilipaswa kununulia dawa na vifaa tiba.
Naibu Waziri Jafo amewataka watumishi wote kusimamia mipango ya serikali ili kutatua kero za wananchi ili kuleta maendeleo katika jamii.
Comments