Friday, July 14, 2017

WAZIRI MKUU AZINDUA MAJENGO YA ZAHANATI YA NNOLELA MKOANI LINDI LILILOKARABATIWA NA KUJENGWA NA NHC

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo kuu la Zahanati, jengo la uzazi na jengo la upasuaji ambayo yote kwa pamoja yamekarabatiwa na kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa kwa agizo alilotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli alipokuwa kwenye ziara ya Mikoa ya kusini tarehe 4/3/2017 na alitoa muda wa miezi mitatu. Yani Zahanati iwe tayari kufikia tarehe 4/06/2017. Mheshimiwa Rais alichangia Sh.ilingi 5,000,000/= ,Mbunge wa Mtama Mheshimiwa Nape Nnauye Sh.10,000,000/= Halmashauri ya Lindi ilichangia Sh.30,000,000/= na NHC kupitia kitengo cha huduma kwa Jamii ilichangia Sh.10,584,634/= pamoja shughuli nzima ya ujenzi. Gharama nzima ya ukarabati na ujenzi huu ni Sh.65,584,634/=.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu huku Mbunge wa Mtama Mheshimiwa Nape Nnauye akishuhudia.
Kaimu Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi, Gibson Mwaigomole akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa juu ya ujenzi na ukarabati uliofanywa na NHC zahanatini hapo.
  Timu ya Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja katika moja ya majengo ya hospitali hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa, Mbunge wa Mtama Mheshimiwa Nape Nnauye, Meneja wa NHC mkoa wa Mtwara, Nehemia Msigwa na Kaimu Meneja wa NHC mkoa wa Lindi, Gibson Mwaigomole wakifuatilia tukio hilo muhimu lililokuwa likiendelea mkoani humo. 
 Sehemu ya Majengo ya Zahanati ya Nnolela yanavyoonekana pichani
Sehemu ya Majengo ya Zahanati ya Nnolela yanavyoonekana pichani
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa akikaribishwa na Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Lindi Gibson Mwaigomole huku Mbunge wa Mtama Mheshimiwa Nape Nnauye akishuhudia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumzia utekelezaji wa mradi wa ukarabati na ujenzi wa hospitali hiyo ulivyofanyika.


 Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Lindi Gibson Mwaigomole akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa.


Post a Comment