Sunday, July 02, 2017

MAVUNDE ATOA RAI KWA BENKI NA TAASISI ZA FEDHA KUSOGEZA HUDUMA ZAO VIJIJINI ILI KUWAHUDUMIA WAKULIMA




Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Anthony Peter Mavunde akizungumza na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yetu Microfinance Ernest Ndimbo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akizungumza jambo na Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, Bwana Millinga.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akielekea eneo la uzinduzi wa Benki hiyo.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akizindua Benki hiyo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akiteta jambo na Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo, Bwana Millinga.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo pamoja na wafanyakazi wa benki ya YETU.

......................................................................
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde amezitaka benki na Taasisi za Fedha kusogeza huduma zao katika maeneo ya Vijijini ili kuwafikia watanzania wengi ambao wanajihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na Ufugaji.

Mavunde alitoa rai hiyo jana wakati wa uzinduzi wa benki ya Yetu Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro kwa kuzitaka Taasisi hizo za fedha zisaidie katika utoaji wa mikopo nafuu kwa wakulima.

Alisema taasisi hizo zitawapatie mikopo ya fedha taslimu,mikopo ya zana za kilimo na mashine za uchakataji wa mazao kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kupitia uchumi wa Viwanda.

Mavunde aliwataka wananchi wa kata ya Mngeta kuitumia hiyo fursa kuboresha kilimo chao kwa kulima kwa njia za kisasa na pia kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya uchakataji mazao.

Aidha,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Bwana Millinga alimuelezea Naibu waziri kwamba wameshaanza mchakato wa kuwakopesha wakulima mashine za uchakataji wa mazao na watatanua wigo zaidi ili kuwafikia wakulima wengi zaidi

No comments: