Moto mkubwa umezuka katika Uwanja wa Ndege wa Songwe jijini Mbeya leo Julai 29, 2017 majira ya mchana na kuzua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa karibu na abiria waliokuwa wakitumia uwanja huo kwa safari zao.
Aidha jitihada za kuuzima moto huo zilifanyika wakati huo nakufanikiwa kuuzima licha ya kuwa ulikuwa umeshaanza kusambaa.
Mamlaka husika haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na chanzo cha moto huo pamoja na madhara yaliyojitokeza kutokana na ajali hiyo.
Tutaendelea kukupa taarifa zaidi juu ya tukio hilo. Tazama picha za tukio.
Comments