Friday, July 07, 2017

Naibu Waziri Ole Nasha awaasa watanzania kula korosho


 Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha akizungumza katika siku ya Korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya Korosho, Makola Majogo akizungumza na waandishi wa habari juu umuhimu wa zao la korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na mifuko ya korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau wa waliofika katika Siku Korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu 
Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda , Gobu ya Jamii 

Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha amewasaa watanzania kula korosho kwa wingi ili kuweza kuepukana na magonjwa mbalimbali ambayo yanagharimu na kukosa nguvu kazi ya taif. 

Nasha ameyasema hayo leo katika Siku ya Korosho katika maonesho ya 41 biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), amesema kuwa korosho inasaidia kuepukana na mafuta mwilini ambayo yanasababisha magojwa ya moyo kwa kiasi kikubwa. 

Amesema kuwa katika utumiaji wa kurosho kwa kula inafanya kuongezeka kwa pato la taifa na kuwafanya wananchi kuwa nguvu kazi yenye kuzalisha kwa tija kwa maendeleo uchumi hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda. 

Nasha amesema kuwa kilimo cha korosho kimeboreshwa na kuwataka wakulima kulima mbegu za kisasa pamoja na kufuata ushauri wa watalaam wa kilimo katika maeneo yao. 

Aidha amesema kuwa katika maonesho hayo watu watumie fursa ya kujifunza kilimo cha kurosho katika kujenga uchumi wa viwanda wa adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Dk. John Pombe Magufuli. 

Makamu Mwenyekiti Bodi ya Korosho, Makola Majogo amesema kuwa wanaendelea katika utoaji wa ulimaji wa kilimo cha kisasa cha kurosho katika kuwa ni zao kuleta maendeleo uchumi wa nchi pamoja na mkulima kunufaika na kilimo hicho

No comments: