Friday, May 01, 2009

Wakili Maira azikwa





JAJI Mkuu Agustine Ramadhani jana ameongoza mamia ya watu katika maziko ya aliyekuwa Wakili maarufu nchini Moses Maira.

Wakili Maira alikuwa ni wakili wa mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya wafanyabiashara watatu wa Mahenge mkoani Morogoro na dereva taksi wa Manzese Abdallah Zombe na pia kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi katika kesi hiyo.

Mwili wa marehemu Maira uliagwa jana katika Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni na heshima za mwisho kutolewa katika ukumbi wa Karimjee, ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria akiwemo Jaji Mkuu Augustine Ramadhani, Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta, Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Pius Msekwa ambaye pia ni Spika wa Bunge mstaafu.

Wengine waliohudhulia katika mazishi hayo ni majaji wa mahakama ya rufaa mawakili wakiongozwa na Rais wa chama cha mawakili (TLS) Fauz Twaib pamoja na Mwenyekiti wa UDP John Cheyo.

Akisoma hotuba fupi iliyoandaliwa na chama cha wanasheria Tanzania Fauz Twaib alisema kuwa Marehemu alikuwa wakili wa 102 kati ya mawakili zaidi ya 1,700 mwenye uzoefu, mahiri na ujuzi mkubwa katika kutetea haki na maslahi kwa wateja wake. imeandaliwa na Martha Ndeki na James Magai. Picha na Fidelis Felix wote wa Mwananchi.

No comments: