Tuesday, May 12, 2009

Usafiri wa Kilwa



Hebu cheki ndugu zetu hawa wanavyotaabika kwa usafiri, hapa wanaonekana wakiwa katika jahazi wakitoka sehemu moja ya bahari ya hindi eneo la Kilwa kwenda nyingine kwa hakika usafiri huu ni mgumu ni hatari na ndiyo maana wiki mbili zilizopita tulishuhudia ndugu zetu wengine wakizama ndani ya bahari ya Hindi na kupoteza maisha, kilio kimekuwa cha muda mrefu na hakipati majibu, hali hii yaendelea kwa wakazi wa visiwani kama vile Mafia, Kilwa na visiwa vingine, ni hatari lakini ni salama maisha yanaendelea watu wanapoteza maisha, lakini hatua kuchukuliwa inakuwa ngumu, Mungu ibariki nchi yetu. Picha ya Said Powa.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...