
Bunge hilo pia limemruhusu Rais Kibaki kuomba msaada wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo mvutano huo utaonekana kutishia usalama wa kanda ya Afrika Mashariki.
Katika hoja hiyo iliyopitishwa na Bunge, wabunge walimtaka Kibaki ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu kutumia mamlaka yake na kufanya kila linalowezekana kulinda ardhi ya Kenya.
Hoja hiyo ambayo juzi ilikosa nguvu baada ya baadhi ya mawaziri kujaribu kuipinga, jana iliweza kupitishwa baada ya serikali kukosa idadi ya kura za kutosha kuipinga.
Wabunge hao walionyesha hisia za wazi wakati wa kujadili suala hilo, wakieleza umuhimu wa kuingia vitani iwapo itabidi, huku wakimtaka Rais Kibaki kuchukua mamlaka kuhusu mipaka ya nchi.
Juhudi za Waziri wa Mambo ya Nje, Moses Wetangula na Waziri wa Habari, Samuel Poghisio kujaribu kupinga hoja hiyo na kujaribu kutafuta upatanishi zaidi zilishindikana. Source: Daily Nation
No comments:
Post a Comment