Sunday, May 24, 2009

matokeo ya awali uchaguzi wa Busanda

Matukio yaliyotufikia yanaonyesha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendeshwa puta na mchuano ni mkali kati ya mgombea wa CCM na yule wa Chadema ambapo katika maeneo ya mjini Katoro Chadema kilionekana kuongoza kwa kura nyingi dhidi ya CCM huku CCM chenyewe kikipimana nguvu katika maeneo ya nje ya mji kwa kuzidiana kura.

Katika maeneo hayo ya vijijini baadhi ya vituo vilivyofikiwa na Mwananchi vilionyesha Chadema kuwa juu sana na CCM kura chache, wakati huo huo vituo vingine vikionyesha CCM ikiwa juu sana na Chadema kupata kura chache.

Katika mji wa Katoro wananchi walikuwa wakishangilia mfululizo huku wakikishangilia chama cha Chadema kwa ushindi, hali hiyo pia ilitokea katika maeneo ya vijijini kwa wafuasi wa CCM.

Hata hivyo Mwenyekiti wa taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema hawezi kusema lolote kwa wakati ule kwani alikuwa akisubiri kwanza matokeo kutoka maeneo ya vijijini ili waweze kujumlishana kumpata mshindi.

Akizungumza na Mwananchi jana Mbowe alisema anasubiri matokeo ya jumla ya uchaguzi huo kwasababu ndiyo utakapo toa mshindi wa uchaguzi huo.

Uchaguzi wa leo umetawaliwa na vituko vya aina mbalimbali, vikiwemo vilivyotokea kwenye mji mdogo wa Katoro, katika eneo la posta ‘B’ kituo cha Ludete ‘B’ ambako wananchi walilizuia gari la Halmashauri ya Wilaya ya Geita (namba za usajili SM 5179) ambalo lilikuwa likitokea kituo cha Shule ya Msingi Mkapa.

Wakiwa wamezuia gari hilo, baadhi yao waliwasiliana na viongozi wa Chadema ambayo ilimtuma mgombea wake, Finias Magesa aliyemkagua mratibu huyo.

“Nimemkagua, hamna taabu. Nimemkagua na nimeridhika hana kitu mwacheni,” alisema Magesa.

No comments: