WAFANYABIASHA Jayant Kumar maarufu kama Jeetu Patel na Devendra Patel wamekiri mahakamani kuwa kampuni ya Bencon Internatinal Limited inayodaiwa kujipatia fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni ya kwao.
Wafanyabiashara hao walikiri hayo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana wakati walipokuwa wakisomewa maelezo ya awali ya kesi yao.
Maelezo hayo yalisomwa na wakili wa serikali Timon Vitalis mbele ya jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo Ruwaich Meela, Grace Mwakipesile na John Kahyoza.
Washitakiwa hao walikiri kuwa wao ni kati ya wakurugenzi wa kampuni hiyo ambayo ilianzishwa hapa nchini Aprili 4 mwaka 2005.
Pia Jeetu Patel na mshitakiwa mwingine Amit Nandy walikubali kuwa kampuni hiyo ilianzishwa hapa nchini Aprili 4 mwaka 2005 na kwamba wao ndio waliokwenda kufungua akaunti benki. Imeandikwa na Nora Damian.
MBIO ZA MWENGE HIZOOOOOOO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasha Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza leo kwa ajili ya kukimbizwa katika Mkoa yote ya Tanzania ambapo jumla ya miradi 138 itakayoharimu jumla ya shilingi 8.6 Bilion itazinduliwa katika mbio za Mwenge mwaka huu, ujumbe wa mwaka huu ni pinga ukatili wa kijinsia wa watoto na Albino. Kulia ni waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Prof Juma Kapuya.
Comments