Thursday, May 21, 2009

Dk Mwakyembe apata ajali mbaya


MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe amepata ajali mkoani Iringa karibu na eneo la Mafinga akiwa njiani akitoka Kyela kuelekea jijini Dar es Salaam, walioshuhudia tukio hilo wanaeleza kuwa gari la Dk Mwakyembe lilipata ajali baada ya kukwepa lori na kisha kutumbukia katika korongo ambapo tairi lilichomoka gari limeharibiwa vibaya na Dk Mwakyembe mwenyewe amekimbizwa hospitalini ambapo anaendelea na matibabu na anaweza kuzungumza kama, lakini haijajulikana ni kiasi gani ameumia.

Tutaendelea kuwaleteeni taarifa zaidi kadri muda unavyokwenda kuhusiana na maendeleo ya kiafya ya Dk Mwakyembe, ambaye amejitokeza siku za karibuni kukabiliana vikali katika vita dhidi ya ufisadi, vita vilivyomuingiza katika malumbano makali na wana- CCM wenzake pamoja na baadhi ya wafanyabiashara.

No comments:

BILIONI 37.7 ZATIKISA TANGA: TARURA YASUKUMA MAPINDUZI YA BARABARA

MAMLAKA ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Tanga imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya baraba...